Qur'ani Tukufu

Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani (Nani Yeye?)

 

102. SURAT AT-TAKAATHUR

(Imeteremka Makka)

 

Sura hii inawaibisha wale ambao kushindania wingi kumewashughulisha na kutimiza yaliyo ya waajibu. Na inawaonya kwamba hakika watakuja jua mwisho wa taksiri yao hiyo, na inawakhofisha watu kuwa watakuja uona Moto na watakuja ulizwa neema walizo kuwa nazo.


KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Kumekushughulisheni kutafuta wingi, Maelezo

2. Mpaka mje makaburini! Maelezo

3. Sivyo hivyo! Mtakuja jua! Maelezo

4, Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua! Maelezo

5. Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini, Maelezo

6. Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu! Maelezo

7. Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini. Maelezo

8. Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.  Maelezo  


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka

Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com

Copyright 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani