Qur'ani Tukufu

Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani (Nani Yeye?)

 

103. SURAT AL-A'S'R

(Imeteremka Makka)

 

Katika Sura hii anaapa Subhanahu kwa Zama, kwa zilivyo kusanya chungu ya ajabu, na mazingatio yenye kujuulisha uweza wa Mwenyezi Mungu na hikima yake, ya kwamba mtu haachi kuwa na upungufu katika vitendo vyake na hali zake ila Waumini wanao tenda mema, na wakausiana kushika Haki. Na hiyo ndiyo kheri yote. Na wakausiana kusubiri na kuvumilia juu ya walio amrishwa na walio katazwa.


KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Naapa kwa Zama! Maelezo

2. Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika khasara, Maelezo

3. Ila wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri.  Maelezo  


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka

Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com

Copyright 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani