Qur'ani Tukufu

Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani (Nani Yeye?)

 

106. SURAT QURAISH

(Imeteremka Makka)

 

Mwenyezi Mungu katika Sura hii anataja neema alizo wafanyia Maqureshi kwa Nyumba yake takatifu ambayo ameilinda na maadui wake, naye akawapa maskani karibu yake wakapata utukufu na amani, na wakawa wanasafiri siku za baridi kwenda Yaman, na siku za joto wakenda Shamu, kwa ajili ya biashara bila ya mtu yeyote kuwaletea maovu, na hali watu jirani zao siku zote wakinyakuliwa. Na neema hizo zinawajibikia kumuabudu huyo aliye kuwa anawalisha wasipate njaa, na akawalinda na khofu.


KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Kwa walivyo zoea Maqureshi, Maelezo

2. Kuzoea kwao safari za siku za baridi na siku za joto. Maelezo

3. Basi nawamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii, Maelezo

4. Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na khofu.  Maelezo  


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka

Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com

Copyright 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani