Qur'ani Tukufu

Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani  (Nani Yeye?)

 

108. SURAT ALKAWTHAR

(Imeteremka Makka)

 

Mwenyezi Mungu katika Sura hii anamtajia Mtume wake s.a.w. neema alizo mfanyia kwa kumpa kheri nyingi na neema kubwa kubwa katika dunia na Akhera, na akamtaka adumishe Sala iliyo safi kwa kumridhi Mwenyezi Mungu, na atoe mhanga bora ya mali yake kwa dhahiya ya shukrani kwa ukarimu alio pewa. Kisha Sura imekhitimisha kwa kumbashiria Nabii s.a.w. kuwa atakatiliwa mbali huyo anaye mchukia na kumbughudhi Mtume.


KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Hakika tumekupa kheri nyingi. Maelezo

2. Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi. Maelezo

3. Hakika anaye kuchukia ndiye aliye mpungufu.  Maelezo


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka

Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com

Copyright 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani