Qur'ani Tukufu

Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani  (Nani Yeye?)

 

110. SURAT ANNAS'R

(Imeteremka Madina)

 

Sura hii imemtaka Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. ukija msaada wa Mwenyezi Mungu na ushindi, na akaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi kwa kutua mambo yake na kutukuka neno lake na kumkamilishia Mwenyezi Mungu, basi amtakase Mola wake Mlezi kwa kumsifu, na amtakase na kila lisio mwelekea, na amwombe msamaha kwa nafsi yake na kwa Waumini, kwa sababu hakika Yeye ni Mwingi wa kukubali toba za waja wake, na anasamehe makosa.


KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi, Maelezo

2. Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi, Maelezo

3. Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba.  Maelezo  


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka

Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com

Copyright 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani