Qur'ani Tukufu

Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani  (Nani Yeye?)

 

112. SURAT AL-IKHLAS'

(Imeteremka Makka)

 

 

Nabii s.a.w. aliulizwa khabari za Mola wake Mlezi, akaamrishwa katika Sura hii ajibu kwamba Yeye ni Mwenye kukusanya sifa zote za ukamilifu, ni Mmoja, wa Pekee, Mwenye kukusudiwa daima katika haja, Mwenye kujitosha hamhitajii yeyote mwenginewe, ametakasika na kuwa na mfano, hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hana  mwenzie katika viumbe vyake.


KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Maelezo

2. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Maelezo

3. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Maelezo

4. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.  Maelezo  


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka

Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com

Copyright 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani