1. Harufi hizi na mfano wa hizi ndizo zikakusanyika kuifanya Qur'ani kuwa ni muujiza ulio washinda watu kuiga mfano wake, ijapo kuwa hizo harufi ndizo wanazo zitamka. Basi mwenye kuitilia shaka hii Qur'ani kuwa imetoka kwa Mwenyezi Mungu au la, basi na alete mfano wake. Na hatoweza.
Rudi kwenye Sura

2. Maneno haya niliyo kufunulia ni Aya za Kitabu chenye kuweka wazi hukumu zote ziliomo ndani yake.
Rudi kwenye Sura

3. Ewe Nabii! Hebu jionee huruma nafsi yako. Usijikere kwa kuhuzunukia inadi ya watu wako, na kuto amini kwao.
Rudi kwenye Sura

4. Sisi tunaweza kuwaletea muujiza wa kuwalazimisha Imani,  wat'ii kwa unyenyekevu amri yake, na yatimie unayo yatarajia. Lakini hatuwaletei, kwa sababu mwendo wetu ni kuwaongoza watu waamini bila ya kuwalazimisha, ili isikosekane hikima ya kujaribiwa kwa mitihani, na yanayo kuja baada yake ya thawabu na adhabu.
Rudi kwenye Sura

5. Wala Mwenyezi Mungu hawaletei watu wako kwa ufunuo wake ya kuwakumbusha Dini ya Haki kuwa ni rehema kwao, ila wao huzua upya upinzani na ukafiri kuukataa. Kwani njia ya uwongofu imekwisha zibwa mbele yao.
Rudi kwenye Sura

6. Hawa hakika wamekadhibisha Haki uliyo ileta, na wakaifanyia maskhara. Lakini wewe wasubirie. Wataona matokeo ya maskhara yao ya kuangamiza.
Rudi kwenye Sura

7. Hivyo hao wanatenda watendavyo katika ukafiri wao na kukadhibisha kwao wala hawaangalii baadhi ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu katika hii hii ardhi? Lau kuwa wanaangalia kwa kuzingatia wangeli ongoka. Hebu wazingatie hii mimea ya kila namna yenye manufaa tunayo itoa Sisi kwenye ardhi, na wala hawezi hayo isipo kuwa Mungu Mmoja Muweza.
Rudi kwenye Sura

8. Hakika katika kutoka kwa hii mimea ni dalili kubwa ya kuwepo Muumba Muweza. Lakini wengi wa watu si wenye kuamini.
Rudi kwenye Sura

9. Hakika Mwenye kumiliki mambo yako, na Mwenye kukulinda, ndiye atakaye waadhibu hao wanao kadhibisha, na ndiye Mwenye kuwafadhili Waumini kwa rehema.
Rudi kwenye Sura

10. Ewe Muhammad! Watajie watu wako kisa cha Musa pale Mola wako Mlezi alipo mwita: Ewe Musa! Nenda kwa Utume kwa watu walio dhulumu nafsi zao kwa ukafiri, na wakawadhulumu Wana wa Israili kwa kuwafanya watumwa na kuwauwa watoto wao wanaume.
Rudi kwenye Sura

11. Nenda kwa kaumu ya Firauni; kwani hao wamepita mipaka katika dhulma yao. Ama ajabu ya watu hawa! Hawaogopi nini litalo wafika kwa vitendo vyao hivi, wakatahadhari?
Rudi kwenye Sura

12. Musa akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi nina khofu wasije kuukataa ujumbe wangu kwa kiburi na inda.
Rudi kwenye Sura

13. Na mimi nimejaa dhiki kwa kuwa wataniambia mwongo, na ulimi wangu si mkunjufu wa kuweza kuhojiana nao kama ninavyo penda.  Basi mtume Jibril ende kwa ndugu yangu aje kuniunga mkono katika hii kazi yangu.
Rudi kwenye Sura

14. Na watu hawa wana kisasi juu yangu. Kwani mimi nilimuuwa mtu katika wao.  Basi nina khofu watakuja niuwa kwa kisasi kabla sijatimiza kazi yangu. Hayo yananizidisha khofu.
Rudi kwenye Sura

15. Mwenyezi Mungu akamwambia: Hawatokuuwa. Na kwa mintarafu ya Haruni nimekukubalia ombi lako. Basi nendeni nanyi mmejizatiti na miujiza yetu. Mimi niko pamoja nanyi kwa ulinzi. Nayasikia yanayo jiri baina yenu na Firauni. Nyinyi mtapata ushindi, na kuungwa mkono.
Rudi kwenye Sura

16. Muelekeeni Firauni na mwambieni: Sisi ni Watume wawili tumetumwa na Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Rudi kwenye Sura

17. Anakwambia Mola Mlezi wa walimwengu wote: Waachilie huru Wana wa Israili, wende nasi.
Rudi kwenye Sura

18. Firauni akamwambia Musa kwa kumsimbulia, naye alimtambua walipo ingia na wakakadimisha Ujumbe wao, kwani alilelewa mle mle katika kasri lake: Hatukukulea sisi ulipo kuwa mtoto? Na ukaishi chini ya ulezi wetu kwa miaka mingi katika umri wako?
Rudi kwenye Sura

19. Na ukatenda makosa yako ya jinaya maovu kumuuwa mtu katika kaumu yangu, na ukazikanusha neema zangu nilizo kufanyia, hukuwahifadhi raia zangu, ukaushambulia ungu wetu kwa kudai kuwa wewe ati ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Rudi kwenye Sura

20. Musa akasema: Niliyafanya uliyo yataja kwa kutojua yanayo faa kutambulikana kwa akili nayo ni jambo la kuuwa. Basi hapana masimbulizi juu yangu.
Rudi kwenye Sura

21. Nikakukimbieni nilipo khofu kuwa mtakuja niuwa kwa jinaya hii ambayo sikuukusudia. Mola wangu Mlezi akanitunukia fahamu na ilimu, kwa fadhila zake na neema zake, na akanifanya mmoja katika Mitume.
Rudi kwenye Sura

22. Musa akaashiria sifa katika sifa ovu kabisa za Firauni, nayo ni kuwa kawafanya watumwa Wana wa Israili, na akiwauwa watoto wao wanaume. Na akakataa kukuita kule kulelewa kwake katika jumba la Firauni kuwa ni neema, kwani yaliyo sabibisha hayo ni yale aliyo kwisha yataja, ndio yeye alitupwa mtoni aokoke asiuliwe. Akaishia kwenye jumba la Firauni. Na lau kuwa si hivyo basi angeli lelewa na wazazi wake.
Rudi kwenye Sura

23. Firauni akasema: Na nini hizo sifa za Mola Mlezi wa walimwengu wote ambaye unakithiri kumtaja, na wewe unadai kuwa ni Mtume wake, na hali sisi hatujui lolote khabari zake?
Rudi kwenye Sura

24. Musa akasema: Yeye huyo ndiye Mwenye kuzimiliki mbingu na ardhi na kila kilio baina yao. Ikiwa nyinyi mna yakini ya ukweli wa jawabu hii basi mtanafiika, na mtaongoka, na mtajua kuwa ufalme wa Firauni wa kujidai haufui dafu mbele ya Ufalme wake Mwenyezi Mungu. Kwani ufalme wa Firauni haupindukii hata eneo moja katika hii dunia.
Rudi kwenye Sura

25. Firauni kuonyesha mastaajabu kwa wale walio mzunguka kwa kuwa Musa katika jawabu yake alipo mtaja Mola wake Mlezi na akadhukuru Ufalme wake hakuugusia hata kidogo ufalme wa Firauni, alisema: Mwayasikiaje maneno ya Musa?
Rudi kwenye Sura

26. Musa akiendelea na usemi wake bila ya kujali hasira za Firauni na uchafu wa maneno yake, akasema: Ndiye huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote, aliye kuumbeni nyinyi na baba zenu walio tangulia. Na miongoni mwa hao walikuwako walio dai ungu kama unavyo dai wewe. Na wao wameteketea. Na wewe utateketea, na hayo unayo yadai yatapotelea mbali. Kwani Mungu wa kweli hafi.
Rudi kwenye Sura

27. Firauni akwaambia watu wake yale yanayo mtibuwa roho na kumghadhibisha, akautaja Utume wa Musa ni kwao wao, wala si kwake yeye, na akambandikiza wazimu, kwa kuwa ati akiulizwa kitu hujibu kingine, na anamsifu Mola Mlezi kwa sifa za kiajabu ajabu. Na kwa hivyo Firauni anawahimiza wamkadhibishe.
Rudi kwenye Sura

28. Musa akasema: Ikiwa nyinyi mna akili, basi uaminini Ujumbe wangu. Kwani kuchomoza jua na kuchwa kwake kwa mpango madhubuti ni dalili wazi ya Mwenye kuumba. Kwa hivyo basi ni nyinyi ndio mnastahiki kuambiwa wendawazimu.
Rudi kwenye Sura

29. Firauni akamwambia Musa: Ukimfuata mungu yeyote badala yangu mimi, utakuwa mmoja katika wanao ijua hali yao mbaya katika magereza yangu. Na yeye Firauni kaangukia kitisho hichi baada ya kushindwa kuondoa athari za kazi za Muumbaji.
Rudi kwenye Sura

30. Musa akasema kwa upole kwa kutumai asaa akaamini: Utanitia gerezani hata nikikuletea ushahidi mkubwa wa ukweli wa haya niyasemayo?
Rudi kwenye Sura

31. Firauni akasema: Ulete ushahidi utao onyesha Unabii wako kama wewe kweli unasema kweli katika wito wako. Kasema hayo kwa tamaa ya kuwa huenda akapata kipengee cha udhaifu katika hoja zake.
Rudi kwenye Sura

32. Musa akaitupa fimbo yake mbele yao. Ikageuka nyoka kweli kweli, si kitu cha uwongo cha uchawi kinacho fanana na nyoka.
Rudi kwenye Sura

33. Musa akautoa mkono wake kutoka mfukoni mwake. Hiyo ni Ishara ya pili.  Nao ukawa mweupe, bila ya maradhi, hata wakashangaa watazamaji kwa kumetuka kwake.
Rudi kwenye Sura

34. Firauni akawaambia watu wake: Hakika Musa ni mchawi bingwa katika uchawi wake. Kasema hayo kwa kuchelea watu wake wasiifuate Haki waliyo iona kwa Musa.
Rudi kwenye Sura

35. Tena Firauni akasema: Mchawi huyu anataka kunifanyia kahari apate kukutoeni katika hii nchi yenu. Na haya ni uchochezi dhidi ya Musa, kwani katika la dhiki mno katika hayo yaliyo dhiki ni mtu kuiacha nchi yake, na khasa ikiwa kwa kahari. Naye akataka mawazo ya wale walio kuwa wanamuabudu. Kasahau ungu wake kwa nguvu za Ishara za Musa.
Rudi kwenye Sura

36. Watu wake wakamwambia: Akhirisha kukata shauri yao hawa, na uwatume askari wende wawakusanye wachawi katika raia zako. Kwani uchawi hupingwa kwa uchawi.
Rudi kwenye Sura

37. Watakuletea wengi, na wote wamebobea kwa uchawi, na wamemshinda Musa kwa ufundi na ustadi. Wamekusudia kwa haya kumpunguzia dukuduku lake Firauni.
Rudi kwenye Sura

38. Wakakusanywa wachawi kutoka kila upande wa nchi. Wakawekewa wakati wa mchana siku ya Sikukuu kukutana na Musa.
Rudi kwenye Sura

39. Na watu wakahimizana kuhudhuria siku hiyo waone ramsa wakiambizana:  Mtakusanyika? Yaani ndio: Mkusanyike!
Rudi kwenye Sura

40. Wakatangaza matarajio yao ya kushinda wachawi, ili wapate kuthibiti katika dini yao, na pia ndio kampeni ya nguvu na juhudi apate kushindwa Musa.
Rudi kwenye Sura

41. Walipo kuja wachawi kwa Firauni walimwambia: Je! Tutapata kwako ujira mkubwa  pindi tukishinda?
Rudi kwenye Sura

42. Firauni akasema: Naam, mtapata mnacho kisema. Na juu ya huo ujira mkubwa mtakuwa watu wa karibu kwangu, watu wa cheo na madaraka.
Rudi kwenye Sura

43. Ulipo fika wakati ulio wekwa katika siku iliyo pangwa Musa aliwaambia wachawi: Tupeni huo uchawi mnao taka kuutupa.
Rudi kwenye Sura

44. Wakazitupa kamba zao na fimbo zao, na watu wakazugwa wakaona kama ni nyoka wanakwenda. Wakaapa kwa utukufu wa Firauni na nguvu zake hapana shaka hawa leo watashinda
Rudi kwenye Sura

45. Musa tena akatupa fimbo yake. Mara ikawa joka kubwa likaingia kuvimeza vile walivyo vizua kwa uchawi, navyo ni kamba na fimbo, wakidanganya kuwa ni nyoka wanao kwenda.
Rudi kwenye Sura

46. Wachawi wakaanguka wakasujudu kumsujudia Mwenyezi Mungu, walipo yakinika kuwa mambo ya Musa si uchawi.
Rudi kwenye Sura

47. Wakasema ili kutia mkazo kule kusujudu kwao kwa kauli yao: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Rudi kwenye Sura

48. Na wakabainisha kuwa hakika Mola Mlezi wa walimwengu wote walio muamini ndiye: Mola Mlezi wa Musa na Harun.
Rudi kwenye Sura

49. Firauni kwa kukasarika kuwa wale wachawi wamemuamini Musa bila ya yeye kuwapa ruhusa, aliwatishia ya kwamba yeye ndiye mwalimu wao aliye wafunza fani za uchawi, na watakuja jua adhabu itakayo wateremkia. Akawaambia: Nitakata mikono yenu na miguu yenu mbali mbali, nitakata wa kulia huu kwa wa kushoto huu, na kinyume cha hayo. Na nyote nitakutundikeni juu ya misalaba.
Rudi kwenye Sura

50. Wachawi wakasema: Hapana la kutudhuru sisi kwa adhabu unazo tutishia, kwani sisi ni wenye kurejea kwenye malipo ya Mola wetu Mlezi. Na Yeye ndiye mbora wa kulipa na mbora wa kuadhibu.
Rudi kwenye Sura

51. Hakika sisi tunataraji Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu tuliyo yafanya zamani, kwa kuwa sisi ndio wa mwanzo wa Waumini katika kaumu yako.
Rudi kwenye Sura

52. Na Mwenyezi Mungu alimpa wahyi Musa a.s. atoke usiku usiku pamoja na Waumini miongoni mwa Wana wa Israili, ilipo kuwa tena haiwi kumsubirisha Musa. Mpango ukawa wa makundi mawili kwamba atangulie Musa na kaumu yake, na Firauni afuatie na kaumu yake, mpaka waingie katika maingilio ya njia ya baharini, na Mwenyezi Mungu awateketeze.
Rudi kwenye Sura

53. Firauni akawatuma askari wake katika miji ya mamlaka yake, wawakusanye wenye maguvu katika kaumu yake, alipo jua kuwa Musa kesha toka na Wana wa Israili, ili awazuie lile walilo kusudia.
Rudi kwenye Sura

54. Firauni akasema: Hakika hawa Wana wa Israili walio kimbia na Musa ni taifa dogo kwa nguvu zao. Idadi yao ni chache. Anasema hayo kutia mori katika nyoyo za askari wake.
Rudi kwenye Sura

55. Na wao juu ya hivyo, wanatutibua roho kwa kuvunja amri yetu na kutoka bila ya idhini yetu.
Rudi kwenye Sura

56. Na sisi ni wengi. Miongoni mwa ada zetu ni kuchukua hadhari, na kuwa macho, na kupania.
Rudi kwenye Sura

57. Tukawatoa Firauni na askari wake kwenye nchi yao iliyo fanana na mabustani yapitiwayo na mito kati yao, wakaangamia kwa kujitenga kwao na Haki, na kuchochewa kutaka kumfuatia Musa, kama ilivyo kuja katika Aya tatu zilizo tangulia.
Rudi kwenye Sura

58. Tukawatoa, kadhaalika, kwenye khazina za dhahabu na fedha, na majumba waliyo kuwa wakiyakalia, wakineemeka kwa uzuri wake na ubora wa starehe zake.
Rudi kwenye Sura

59. Ni kutoka kama huku kwa ajabu tulivyo kueleza ndivyo tulivyo watoa, na tukawapa  ufalme huo na kila namna ya neema zilizo kuwamo Wana wa Israili, baada ya kuwa masikini hawana mbele wala nyuma.
Rudi kwenye Sura

60. Firauni na watu wake wakakaza mwendo ili wapate kuwawahi Wana wa Israili. Wakawakuta wakati wa kuchomoza jua.
Rudi kwenye Sura

61. Walipo onana makundi mawili, watu wa Musa walisema: Hakika Firauni na watu wake watatupata. Basi tutaangamia.
Rudi kwenye Sura

62. Musa akasema: Hakika mimi ninao uangalizi wa Mwenyezi Mungu unao nifuata kwa kunihifadhi. Na Yeye ataniongoza kwenye Njia ya uwokovu. Amesema hayo ili awatuze kuwa watasalimika, na iwe mbali na mawazo yao fikra ya kutisha kwamba watakuja patikana.
Rudi kwenye Sura

63. Tukamuamrisha Musa kwa wahyi, ufunuo, aipige bahari kwa fimbo yake. Ikapasuka bahari njia kumi na mbili kwa mujibu wa idadi ya mataifa ya Wana wa Israili. Kila njia katika hizo njia ilikuwa na kizuizi cha maji yaliyo nyanyuka kama mlima ulio simama imara.
Rudi kwenye Sura

64. Tukawajongeza Firauni na kaumu yake mpaka wakaingia kwenye zile njia nyuma ya Musa na kaumu yake.
Rudi kwenye Sura

65. Tukamwokoa Musa na walio kuwa pamoja naye kwa hifadhi ya bahari nayo imeshikamana, mpaka wakamalizika kuvuka.
Rudi kwenye Sura

66. Kisha tukamzamisha Firauni pamoja na walio kuwa pamoja naye kwa kuwafudikiza kwa maji pale walipo wafuata.
Rudi kwenye Sura

67. Hakika katika vituko hivi vya ajabu vya kiungu pana funzo la kuzingatia kwa atakaye kunafiika. Lakini watu wengi si wenye kusadiki.
Rudi kwenye Sura

68. Hakika Muumba wako na Mlezi wako ndiye huyo Mwenye nguvu katika kuwaadhibu wanao kanusha, Mwenye kuwaneemesha kwa rehema Waumini.
Rudi kwenye Sura

69. Ewe Mtume! Na wasomee makafiri hadithi ya Ibrahim , Alayhi Ssalaam.
Rudi kwenye Sura

70. Alipo mwambia baba yake: Mnaabudu kitu gani hichi, ambacho hakifai kuabudiwa?  Anakusudia kwa hayo kuyakebehi masanamu.
Rudi kwenye Sura

71. Wakasema kujibu kwa njia ya kujitapa: Tunaabudu masanamu, nasi tunadumu daima dawamu tukiyaabudu, kwa kuyaadhimisha na kuyatukuza!
Rudi kwenye Sura

72. Ibrahim akasema: Kwani yanasikia madua yenu? Au yanakuitikieni mnapo yaomba? Kwa hayo anakusudia kuwanabihisha upotovu wa mwendo wao.
Rudi kwenye Sura

73. Au yanakuleteeni manufaa mnapo yat'ii? Au yanakupatilizeni kwa madhara mkiyaasi?
Rudi kwenye Sura

74. Wakasema: Hawafanyi lolote katika hayo. Lakini sisi tumewakuta baba zetu wakiyaabudu mfano wa ibada yetu. Basi sisi tukawafwata  kwa waliyo kuwa wakiyafanya.
Rudi kwenye Sura

75. Ibrahim akasema kwa kuwasusuika: Je! Mlifikiri hata mkalijua jambo lolote lilio kupelekeeni kudumu na kuyaabudu hayo masanamu?
Rudi kwenye Sura

76. Nyinyi na baba zenu wa zamani - ati haya yanastahiki kuabudiwa au la? Lau mngeli zingatia mngeli jua kuwa hakika nyinyi mko katika upotovu ulio wazi.
Rudi kwenye Sura

77. Kwani hakika hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni maaadui kwangu mimi na kwenu. Basi mimi siwaabudu hao. Lakini ninaye muabudu na najijongeza kwake ni Muumba wa walimwengu wote, na Mwenye kumiliki mambo yao, na Mwenye kuwalinda.
Rudi kwenye Sura

78. Ambae ndiye aliye nizua kabla sijawa chochote akaniumba kwa bora ya umbo, na akanitunukia uwongofu wa kunifikishia kwenye mafanikio yangu ya duniani na Akhera.
Rudi kwenye Sura

79. Na Yeye ndiye aliye nineemesha kwa vyakula na vinywaji, na akaniwezesha kuvipata na kunafiika kwavyo, ili kuhifadhi uhai wangu.
Rudi kwenye Sura

80. Na yakinishukia maradhi ni Yeye ndiye anaye niponesha, kwa kunisahilishia sababu za kupona na kuniwezesha kuzipata.
Rudi kwenye Sura

81. Na Yeye ndiye atanifisha ikifika ajali yangu, na tena atanihuisha mara nyengine kwa ajili ya hisabu na malipo.
Rudi kwenye Sura

82. Na Yeye ndiye ninaye mtumai kunighufiria na kuyasemehe makosa yangu madogo madogo ya kujikwaa  duniani, utapo fika wakati wa hisabu.
Rudi kwenye Sura

83. Ibrahim a.s. akasema kwa kuomba: Mola wangu Mlezi! Nitunukie ukamilifu wa ilimu na vitendo, ili nipate kustahili kuubeba Ujumbe wako na hukummu kwa waja wako, na niwezeshe niungane pamoja na kundi la watendao wema.
Rudi kwenye Sura

84. Na nijaalie nipate sifa nzuri na kumbusho jema kwa kaumu zitazo kuja baada yangu, mabaki yake yasalie mpaka Siku ya Kiyama.
Rudi kwenye Sura

85. Na nijaalie katika waja wako ulio watunukia neema za Peponi, kuwa ni malipo kwa sababu ya Imani yao kukuamini Wewe, na ibada yao kukuabudu Wewe.
Rudi kwenye Sura

86. Na mjaalie baba yangu astahili msamaha kwa kumwezesha kuwa Muislamu.  Na yeye alikuwa kamuahidi kusilimu siku alio achana naye, kwani yeye huyo baba alikuwa ameitupa kando njia ya uwongofu na uwongozi.
Rudi kwenye Sura

87. Wala usinitie aibu au hizaya mbele ya watu, Siku watapo tolewa makaburini kwa ajili ya hisabu na malipo.
Rudi kwenye Sura

88. Siku ambayo hapana mtu ataye nafiika kwa mali ayatoe, au kwa wana wamsaidie.
Rudi kwenye Sura

89. Isipo kuwa aliye kuwa Muumini, na akamkabili Mwenyezi Mungu na moyo ulio mzima, hauna maradhi ya ukafiri, na unaafiki, na riya  (kujionesha).
Rudi kwenye Sura

90. Na Pepo itajongezwa, na itakaribishwa pahala pa watu wema. Basi wataiendea wale walio jikinga na ukafiri na maasi, na wakaikubali Imani na ut'iifu duniani.
Rudi kwenye Sura

91. Na Moto utaletwa mbele ya walio iacha Dini ya Haki, mpaka ndimi zake zikaribie kuwanyakua, nao watakuwa majutoni.
Rudi kwenye Sura

92. Wakaambiwa kwa kuwatahayarisha: Iko wapi hiyo miungu yenu mliyo kuwa mkiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu?
Rudi kwenye Sura

93. Badala ya Mwenyezi Mungu, na mnadai kuwa ati ndio itakuombeeni hii leo? Je! Inakufaeni kitu kwa kukunusuruni,  au hata inajifaa wenyewe kujisaidia? Hapana lolote. Kwani wao na miungu yao ni kuni za Moto.
Rudi kwenye Sura

94. Watatumbukizwa katika Jahannamu kifudifudi, wakipinduliwa pinduliwa mpaka waishie ndani kabisa shimoni, wao na walio wapoteza na wakawatia katika madhambi na upotovu.
Rudi kwenye Sura

95. Na pamoja nao watakuwapo wasaidizi wa Ibilisi walio kuwa wakiwapambia shari na madhambi, au wale watu na majini walio wakiwafuata katika maasi.
Rudi kwenye Sura

96. Watasema huku wakiungama makosa yao, na huku wanagombana na miungu yao waliyo kuwa wakiiabudu:
Rudi kwenye Sura

97. Wallahi! Hakika sisi tulikuwa katika dunia yetu tumepotea kweli, na wajinga wa kutupwa, na tumeiacha Haki ambayo haina kificho ndani yake.
Rudi kwenye Sura

98. Pale tulipo kufanyeni nyinyi tulio kuabuduni badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ati ni sawa sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote katika kustahiki kuabudiwa, juu ya kuwa hamjiwezi wala hamfai kwa lolote.
Rudi kwenye Sura

99. Wala hapana walio tutia katika hilaki hii ila wakosefu walio tupotoa tukaiwacha Njia Iliyo Nyooka.
Rudi kwenye Sura

100. Basi hapana wa kuombwa akaja kutuvua na adhabu hii kama tulivyo dhania pale kwanza.
Rudi kwenye Sura

101. Wala hapana rafiki wa kuwaonea uchungu kwa hali yao,  licha ya kuwaokoa.
Rudi kwenye Sura

102. Basi hapo ndio wanajitamania nafsi zao lau wangeli rejea duniani wapate kuwa Waumini ili waokoke.
Rudi kwenye Sura

103. Na hakika katika khabari za Ibrahim zilizo tajwa yapo mawaidha na mazingatio kwa mwenye kutaka mawaidha na akazingatia. Na wala si wengi katika watu wako wanao somewa khabari hizi wenye kuitikia wito wako.
Rudi kwenye Sura

104. Na hakika hapana shaka Mola wako Mlezi ni Muweza wa kuwaadhibu wanao kadhibisha, naye ni Mfadhili wa watu wema kwa neema nyingi.
Rudi kwenye Sura

105. Na Mwenyezi Mungu ametaja khabari za Nuhu kwa kauli yake: Kaumu ya Nuhu iliukanusha Utume wake, wakamrudishia mwenyewe. Kwa kitendo hicho ikawa wamewakadhibisha Mitume wote wa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa wito wao ni mmoja katika asli yake na lengo lake.
Rudi kwenye Sura

106. Waliukanusha Utume huu pale alipo waambia ndugu yao Nuhu - ndugu kwa makhusiano ya nasaba si kwa Dini - akiwahadharisha: Hamumchi Mwenyezi Mungu, mkaacha kuabudu wenginewe?
Rudi kwenye Sura

107. Hakika mimi ni Mtume, nimetumwa kwenu nikuongoeni kwenye Njia ya wongofu, na ni muaminifu wa kufikisha huu Ujumbe.
Rudi kwenye Sura

108. Basi mkhofuni Mwenyezi Mungu, na fuateni amri yangu katika hayo ninayo kuitieni kwayo ya kumuamini Mwenyezi Mungu wa pekee na kumt'ii.
Rudi kwenye Sura

109. Na wala sitaki kwenu ujira kwa ajili ya ninayo kupeni ya nasaha na wito. Na sina malipo ila kwa Mwenye kuwaumba viumbe wote, Aliye miliki mambo yao.
Rudi kwenye Sura

110. Basi tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na fuateni ninayo kuamrisheni.
Rudi kwenye Sura

111. Watu wa Nuhu, huku wakiukataa wito wake, walisema: Hatutokuwa na imani nawe maadamu wanakufuata watu duni kabisa, wasio kuwa na hadhi wala mali.
Rudi kwenye Sura

112. Nuhu akasema: Kitu gani cha kunijuvya uchache wa hadhi yao na mali yao? Nikitakacho mimi kwao ni Imani yao bila ya kutafuta kuzijua kazi zao.
Rudi kwenye Sura

113. Hapana wa kuwalipa kwa vitendo vyao na kazi zao ila Mola wangu Mlezi;  kwani Yeye ndiye anaye yajua vyema ya undani wao. Kama nyinyi ni watu watambuzi mngeli tambua hayo.
Rudi kwenye Sura

114. Wala mimi siye wa kuwafukuza watu wanao uamini wito wangu vyovyote itavyo kuwa hali yao ya ufakiri au utajiri, kwa sababu ati ya kukubalieni nyinyi kwa mtakalo ili ndio mpate kuniamini.
Rudi kwenye Sura

115. Mimi si chochote ila ni Mtume niliye toka kwa Mwenyezi Mungu  kuwaonya walio wajibikiwa kwa onyo lilio wazi, kwa ushahidi wa kutenganisha baina ya kweli na uwongo, bila ya farka yoyote baina ya mtukufu na mnyonge. Basi vipi itanifalia mimi kuwafukuza Waumini kwa sababu ya ufakiri wao?
Rudi kwenye Sura

116. Wakasema: Ewe Nuhu! Ikiwa hutoacha huu wito wako basi jua yakini tutakupopoa mawe. Yaani wanakusudia kwa haya kumtishia kumuuwa.
Rudi kwenye Sura

117. Nuhu kuonyesha kushikilia watu wake kuukadhibisha wito wake, alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha! Kuthibitisha kuwa wanastahiki maapizo yake.
Rudi kwenye Sura

118. Basi tuhukumie baina yangu na wao, kwa hukumu ya kuwaangamiza wanao pinga Upweke wako, na wakamkadhibisha Mtume wako! Na niokoe mimi na Waumini walio pamoja nami na adhabu ya uasi wao.
Rudi kwenye Sura

119. Ndio hivyo tukamwokoa yeye pamoja na walio amini katika safina iliyo pakia pomoni wao hao pamoja na mahitaji yao, kwa kuitikia dua yake.
Rudi kwenye Sura

120. Baada ya kuokoka kwa Nuhu na walio amini, Mwenyezi Mungu aliwazamisha walio baki katika kaumu ya Nuhu walio kuwa hawakuamini.
Rudi kwenye Sura

121. Hakika katika yaliyo simuliwa na Qur'ani juu ya khabari za Nuhu  ni hoja ya kuthibitisha ukweli wa Mitume na uwezo wa Mwenyezi Mungu. Na katika watu walio somewa hadithi hizi si wengi walio amini.
Rudi kwenye Sura

122. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu za kumuadhibu kila jabari mwenye inda, Mwenye kuwaneemesha wachamngu kwa kila namna ya fadhila.
Rudi kwenye Sura

123. Kabila ya A'di ilimkanusha Mtume wao Hud a.s. Na kwa hivyo wakawa ndio wamewakadhibisha Mitume wote, kwa kuwa wito wao ni mmoja katika asli yake na lengo lake.
Rudi kwenye Sura

124. Alipo waambia ndugu yao Hud: Hamumwogopi Mwenyezi Mungu, mkamsafia ibada?
Rudi kwenye Sura

125. Hakika mimi nimetumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili nikuongoeni mfuate uwongozi, na ni mwenye kuulinda ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Naufikisha ujumbe huo kama alivyo niamrisha Mola wangu Mlezi.
Rudi kwenye Sura

126. Basi ifuateni amri ya Mwenyezi Mungu.  Na ikhofuni adhabu yake. Na t'iini ninayo kuamrisheni yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye Sura

127. Wala kwa hii nasaha yangu na uwongozi wangu sitaki kwenu ujira. Sina malipo isipo kuwa kwa Muumba wa viumbe vyote.
Rudi kwenye Sura

128. Je! Mnasimamisha juu ya kila pahala palipo nyanyuka katika nchi jengo refu kwa ajili ya kujifakhirisha, na mnakutana humo kwa mambo ya upuuzi na fisadi? Mwenyezi Mungu Subhanahu anataka kwa haya kuwazindua watende yatakayo wanufaisha, na anawatahayarisha kwa kuacha kwao Imani na vitendo vyema.
Rudi kwenye Sura

129. Na mnajenga majumba ya fakhari na imara, na mahodhi ya maji, kwa kutaraji kuishi milele katika dunia hii, kama kwamba hamtakufa.
Rudi kwenye Sura

130. Na mnapo ingia kutesa, mnapita kiasi katika uasi na uvamizi wa jeuri, mnauwa, na mnapiga  kwa chuki bila ya huruma.
Rudi kwenye Sura

131. Mwogopeni Mwenyezi Mungu katika kutumia nguvu, Na fuateni amri yangu katika ninayo kuitieni. Kwani hayo hakika ndiyo yatakayo kukufaeni na ndiyo yatakayo dumu zaidi.
Rudi kwenye Sura

132. Na tahadharini na ghadhabu za Mwenyezi Mungu aliye kukunjulieni neema zake, kwa mnayo yajua yaliyo mbele yenu ya vipawa vyake vya namna mbali mbali.
Rudi kwenye Sura

133. Kama alivyo kupeni mifugo kama ngamia, na ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, na wana wenye nguvu, wakukulindieni mifugo yenu, na kukusaidieni katika shida za maisha.
Rudi kwenye Sura

134. Na mabustani yenye matunda, na chemchem zenye kutiririka maji mnayo yahitajia.
Rudi kwenye Sura

135. Mimi nina khofu asije Mwenyezi Mungu akakuteremshieni adhabu kali hapa duniani, na Akhera akakutieni katika Moto wa Jahannamu kwa sababu ya ujabari wenu na starehe alizo kustarehesheni Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye Sura

136. Wakasema kwa kumkejeli: Ni sawa kwetu, ukitupa waadhi na kutuonya au ukawa si katika wenye kutoa waadhi.
Rudi kwenye Sura

137. Haya uliyo tuletea si lolote ila ni uwongo na upotovu wa watu wa zamani. Wao wamezoea kuzua kama hivyo. Kwa hivyo sisi hatutaacha tuliyo kuwa nayo.
Rudi kwenye Sura

138. Wala sisi hatutaadhibiwa kwa vitendo tuvitendavyo.
Rudi kwenye Sura

139. Basi wakaendelea kushikilia kumkanusha. Mwenyezi Mungu akawafanyia haraka kuwateketeza. Hakika katika hayo aliyo wateremshia Mwenyezi Mungu kina A'di kwa kuwa ni malipo kwa ukanushi wao, ni hoja inayo juulisha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Na si wengi katika wanao somewa khabari za A'adi walio Waumini.
Rudi kwenye Sura

140. Na Mola wako Mlezi ndiye Mtenda nguvu wa kuwashinda hao majabari, Mwenye kuwarehemu Waumini.
Rudi kwenye Sura

141. Kabila ya Thamud ilimkanusha Saleh katika Ujumbe wake na wito wake, na kwa hivyo ikawa wamewakanusha Mitume wote, kwa kuwa asli ya Ujumbe ni moja, na lengo ni moja.
Rudi kwenye Sura

142. Ewe Mtume! Watajie watu wako, wakati ule kina Thamud walipo ambiwa na ndugu yao kwa uzao na uwananchi, si kwa dini, Saleh: Hamumwogopi Mwenyezi Mungu, mkamuaabudu Yeye tu?
Rudi kwenye Sura

143. Hakika mimi nimetumwa na Mwenyezi Mungu kwenu kwa mambo yenye kheri yenu na mafanikio yenu. Na mimi ni mwenye kuuhifadhi Ujumbe huu kama nilivyo upokea kwa Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye Sura

144. Kwa hivyo tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na nifuateni kwa haya ninayo kuitieni kwayo kutokana na amri zake.
Rudi kwenye Sura

145. Wala sitaki kwenu ujira wowote kwa hii nasaha yangu na uwongozi wangu. Ujira wangu uko kwa Mwenye kumiliki walimwengu wote.
Rudi kwenye Sura

146. Lilio wazuia ni kule kuamini kwao kwamba ati wataselelea katika zile starehe, watasalimika na adhabu, na kutoweka, na mauti,
Rudi kwenye Sura

147. Katika mabustani ya matunda, na chemchem zenye kutoa maji matamu,
Rudi kwenye Sura

148. Na konde zilizo wiva, na mitende ambayo mazao yake yamedhihiri mapevu na laini.
Rudi kwenye Sura

149. Na mnachonga milimani majumba kwa ufundi na ustadi katika hayo mnayo yaunda.
Rudi kwenye Sura

150. Basi iogopeni adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kuto mshukuru kwenu kwa neema zake; na pokeeni nasiha yangu na muitende.
Rudi kwenye Sura

151. Wala msiit'ii amri ya walio pindukia mipaka kwa ushirikina na kufuata pumbao na matamanio.
Rudi kwenye Sura

152. Ambao wanapitisha maisha yao katika ardhi kwa uharibifu, wala hawafanyi ya maslaha ya kutengeneza nchi.
Rudi kwenye Sura

153. Wakasema: Wewe si chochote isipo kuwa miongoni mwa walio rogwa kikweli mpaka zikapotea akili zao. Na katika jawabu hii mna ukali na usafihi.
Rudi kwenye Sura

154. Wewe si chochote ila ni mmoja unaye fanana na sisi kwa ubinaadamu, basi yawaje uwe bora kuliko sisi kwa Unabii na Utume? Na ukiwa wewe ni mkweli katika madai yako basi lete muujiza wa kuonyesha uthibitisho wa Utume wako.
Rudi kwenye Sura

155. Saleh akawaambia - alipo pewa na Mwenyezi Mungu ngamia jike kuwa ni muujiza wake: Huyu hapa ngamia jike wa Mwenyezi Mungu, amekutoleeni kuwa ni Ishara. Yeye ana sehemu yake ya maji katika siku moja; siku hiyo msinywe nyinyi. Na nyinyi mna sehemu yenu siku nyengine. Kunyweni siku hiyo.
Rudi kwenye Sura

156. Wala msimletee madhara yoyote huyu ngamia, msije mkahiliki kwa adhabu kubwa.
Rudi kwenye Sura

157. Wakamchinja ngamia, kinyume na walivyo wafikiana na Saleh. Kwa hivyo wakastahiki kuwashukia adhabu, wakawa ni wenye kujuta kwa kitendo chao hicho.
Rudi kwenye Sura

158. Basi ikawateketeza adhabu aliyo waahidi Saleh, wala majuto hayakuwakinga na adhabu ya ukosefu wao. Hakika katika kusimulia kisa chao pana dalili ya kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu kuwateketeza makafiri na kuwaokoa Waumini. Na si wengi katika watu wako wenye kuamini.
Rudi kwenye Sura

159. Na hakika bila ya shaka aliye kuumba ndiye Yeye Muweza wa kuwateketeza wapinzani, na Mfadhili wa kuwaokoa wachamngu.
Rudi kwenye Sura

160. Alipo waita Lut'i watu wake wamuabudu Mwenyezi Mungu pekee, na waache ushirikina, waliwakanusha Mitume wote.
Rudi kwenye Sura

161. Ewe Mtume! Watajie watu wako pale Lut'i alipo waambia watu wake, naye ni ndugu yao na shemeji yao:
Rudi kwenye Sura

162. Hakika mimi nimetumwa kwenu na Mwenyezi Mungu nikuleteeni Dini ya Haki. Nami ni muaminifu wa kuifikisha Dini hii.
Rudi kwenye Sura

163. Basi tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na ifuateni amri yangu kwa ninayo kuitieni.
Rudi kwenye Sura

164. Wala mimi sitaki kwenu ujira kwa uwongofu na uwongozi ninao kuitieni. Sina ujira ila kwa Mwenye kumiliki viumbe vyote na Mlezi wao.
Rudi kwenye Sura

165. Lut'i alisema: Nyinyi mnastarehea kuwaingilia wanaume mkaacha wanawake? Kwa hayo anakusudia kuyakanya yale waliyo yazoea ya vitendo vichafu.
"Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?" Yaani kazi ya liwat'i, ambayo tangu asli yake ni ukosefu muovu, unao chusha hata kuusikia, kinyume na maumbile, unao mteremsha mwanaadamu chini kabisa. Na lau kuwa unaenea basi huharibu sunna ya kuoa, nayo ni sunna ya maumbile, hata uzazi ukatike na ulimwengu usite kuendelea.
 Na kwa liwat'i huenea maradhi kama yanavyo enea kwa uzinzi kama tego, kisonono, donda ndugu, maradhi ya ngozi kama ukurutu, na hutokea ishara za kudhoofika nyama za nyuma hata ikawa mtu hawezi kujizuia kutokwa na choo ovyo. Na nyuma kwake mtu huchanua kukawa kama mdomo wa tarumbeta. Na huko nyuma hujaa vijidudu vya maradhi na hivyo humuambukiza mwenye kumuingilia na yeye hivyo vijidudu vikenda mletea maradhi mengine ya njia za mkojo. Na huenda huyo mwenye kufanywa mambo hayo akawa mpumbavu hafai kitu, ikiwa kaanza tangu utotoni. Na huenda akajidai kuonesha ujanadume mwingi kuliko kiasi kwa kutaka kuficha upungufu wake wa uume. (Karibuni imedhihiri kuwa maradhi ya khatari kabisa ya AIDS [Ukimwi] yameenea zaidi sana kwa watendao kitendo hichi na watumiao madawa ya ulevi, ijapo kuwa na wazinzi nao hupata!).
Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ameukemea ukosefu huu katika Aya kadhaa wa kadhaa, na akabainisha hikima ya Mwenye kuhukumu kwa kuharimisha huku, kwa kusema: " Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?  Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!"
Rudi kwenye Sura

166. Na mnaacha aliyo kuumbieni Mwenyezi Mungu ya kustarehe na wake zenu walio halali yenu? Ama hakika nyinyi ni watu mlio pindukia mipaka ya udhalimu katika kufanya maasi.
Rudi kwenye Sura

167. Walikasirika kwa kule kuwakataza na kuwakemea kwa sababu ya jambo ovu na wakasema: Kama hukuacha kutukebehi tutakutoa mji kwa izara kubwa.
Rudi kwenye Sura

168. Lut'i akasema: Hakika mimi nakichukia mno hichi kitendo chenu, wala sitoacha kabisa kukipinga na kukikebehi.
Rudi kwenye Sura

169. Na akamwomba Mola wake Mlezi amwokoe yeye na ahali zake na wayatendayo wale wajinga, baada ya kwisha kata tamaa kuwa hawamsikilizi.
Rudi kwenye Sura

170. Mwenyezi Mungu akamuitikia ombi lake, akamwokoa yeye na wale walio fuata wito wake, kwa kuwatoa wote majumbani mwao wakati wa kuteremka adhabu kuwashukia wenye kukanusha.
Rudi kwenye Sura

171. Ila mkewe kizee aliye baki, na hakutoka nao. Yeye akaangamia kwa kufuru zake na ukhaini wake, kwa kuwaunga mkono wakosefu.
Rudi kwenye Sura

172. Kisha Mwenyezi Mungu akawahiliki makafiri watendao uovu kwa hilaki kali na mbaya.
Rudi kwenye Sura

173. Na Mwenyezi Mungu aliwateremshia wale watu wapotovu mawe kutoka mbinguni, yakawateketeza. Na ilikuwa mvua ya kutisha kwa wingi wake na namna yake. Basi mvua ovu ya walio kwisha onywa ni mvua hiyo, kwani iliteremka kwa uangamizi mkubwa mno!
Rudi kwenye Sura

174. Hakika adhabu ile iliyo wateremkia watu wale hapana shaka ni hoja yenye kuonyesha utimilivu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Wala si wengi katika watu wako wenye kusadiki hayo.
Rudi kwenye Sura

175. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye kusifika kwa rehema iliyo kamilika. Huwapa adhabu watendao dhambi, na huwalipa wema Waumini.
Rudi kwenye Sura

176. Hichi kisa cha Shuaibu pamoja na Watu wa Al Aykat, Machakani, nao ni msitu wenye miti mizuri, karibu na Madian. Kikundi cha watu waliteremkia hapo na wakakaa. Mwenyezi Mungu akawapelekea Shuaibu kama alivyo wapelekea watu wa Madian. Wakamkadhibisha katika wito wake. Na kwa hivi wakawa wamekanusha risala za Mitume wote.
Rudi kwenye Sura

177. Ewe Muhammad! Watajie watu wako pale Shuaibu alipo waambia watu wa Machakani: Je! Hamumkhofu Mwenyezi Mungu mkamuamini? Wakaingia kumkadhibisha.
Rudi kwenye Sura

178. Hakika mimi nimetumwa na Mola Mlezi wa walimwengu wote nikuongoeni na nikuongozeni. Nami ni muaminifu wa kuufikisha ujumbe wake kwenu.
Rudi kwenye Sura

179. Basi tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na nit'iini kwa kufuata amri za Mwenyezi Mungu, na kuziokoa nafsi zenu na madhambi.
Rudi kwenye Sura

180. Na mimi kwa hivi kukuongozeni na kukufunzeni sikutakini ujira wowote. Mimi sina malipo kaamili kwa sababu ya kazi yangu ila kutokana na Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Rudi kwenye Sura

181. Shuaibu akawaamrisha kutimiza vipimo kwa ukamilifu wanapo pima, kwani ilikuwa ada yao kupunguza kwa pishi na mizani, kupunguza haki za watu kwa kuwapunja na kuwapimia kasoro.
Rudi kwenye Sura

182. Na wapimieni watu kwa mizani ya sawa sawa, ili wachukue haki yao kwa uadilifu ulio nyooka.
Rudi kwenye Sura

183. Wala msiwapunguzie watu haki zao, wala msipite katika nchi mkifisidi kwa kuuwa, na uharamia, na kufanya madhambi, na kufuata pumbao.
Rudi kwenye Sura

184. Na tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu aliye kuumbeni, na akaumba kaumu zenye nguvu na takaburi zilizo tangulia.
Rudi kwenye Sura

185. Wakasema: Wewe si chochote ila ni mtu aliye sibiwa na uchawi mkali na ikapotea akili yake.
Rudi kwenye Sura

186. Na wewe si chochote ila ni mmoja wetu sawa na sisi kwa utu. Basi vipi ujipe ubora kuliko sisi kwa Utume? Nasi tunaamini kuwa wewe ni mwongo wa kubobea.
Rudi kwenye Sura

187. Basi hebu tuangushie vipande vya adhabu kutoka mbinguni ikiwa ni katika wasemao kweli kwa huu ujumbe wako!  Na chini ya shauri hii kwa hakika pana kila namna ya ubishi.
Rudi kwenye Sura

188. Shuaibu akasema: Mola wangu Mlezi ni Mjuzi, upeo wa kujua, wa maasi yote myatendayo, na adhabu mnayo stahiki. Yeye atakuteremshieni hayo kwa wakati wake alio ukadiria. Na huu ndio hadi ya mwisho wa kumwachilia Mwenyezi Mungu kila kitu, na kuwatisha hao makafiri.
Rudi kwenye Sura

189. Lakini wao waliendelea kumkadhibisha. Mwenyezi Mungu akawapatiliza kwa adhabu ya joto kuu mno. Wakawa wanatapa tapa hawana pa kukimbilia. Walipo pata kiwingu cha kuwapa kivuli kukinga mwako wa jua walijikusanya chini yake. Mwenyezi Mungu akawateremshia moto, ukawateketeza wote katika siku ya kitisho kikubwa mno.
Rudi kwenye Sura

190. Hakika adhabu iliyo wateremkia watu wa Machakani kuwa ni malipo ya uasi wao, ni dalili ya ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Na hawakuwa wengi wa watu wako wenye kusadiki.
Rudi kwenye Sura

191. Na hakika Mola wako Mlezi hapana shaka ndiye Yeye aliye tengeka kwa Nguvu na Ushindi, Mwenye kuwaneemesha Waumini kwa rehema nyingi.
Rudi kwenye Sura

192. Na hakika hii Qur'ani iliyo tajwa ndani yake visa vya kweli imeteremshwa kutoka kwa Mwenye kuumba walimwengu wote, Mwenye kumiliki mambo yao, na Mlezi wao. Basi khabari zake ni za kweli. Na hukumu yake inatimizwa mpaka Siku ya Kiyama.
Rudi kwenye Sura

193.  Ameiteremsha Roho muaminifu, naye ni Jibril a.s.,
Rudi kwenye Sura

194. Juu ya moyo wako ulio tulia kuihifadhi na kuifahamu, na idhibitike katika moyo wako iwe madhubuti isisahaulike, ili upate kuwaonya wakhalifu kwa adhabu ziliomo ndani yake.
Rudi kwenye Sura

195. Jibril amekuteremshia kwa lugha ya Kiarabu, yenye maana wazi, yenye hoja zilizo dhaahiri kwa wanayo hitajia ya kutengeneza mambo yao ya dunia na Dini.
Rudi kwenye Sura

196. Na hakika kuitaja Qur'ani na kueleza kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu kumteremshia Muhammad s.a.w. yametajwa katika  Vitabu vya Manabii walio tangulia.
Rudi kwenye Sura

197. Je! Hawa wenye inda wanaikataa Qur'ani na hali wao wanayo hoja inayo onyesha ukweli wa Muhammad s.a.w., nayo ni  ilimu ya wanazuoni wa Wana wa Issraili juu ya Qur'ani kama ilivyo katika vitabu vyao?
Rudi kwenye Sura

198. Na lau tungeli mteremshia mtu asiye kuwa Mwaarabu, anaye weza kusema Kiarabu lakini si kwa ufasihi, wasingeli waza kumtuhumu kuwa kaizua.
Rudi kwenye Sura

199. Na angeli wasomea baraabara kinyume na ada bado wangeli mkanusha, na wakapatia kisababu kwa ukafiri wao.
Rudi kwenye Sura

200. Sisi tumekutia huko kukanusha katika nyoyo za wakosefu;  na tumekuthibitisha kama tulivyo kuthibitisha katika nyoyo za wenye sifa kama zao.
Rudi kwenye Sura

201. Basi hapana njia ya wao kuacha tabia yao ya ukafiri mpaka wateseke kwa hiyo adhabu kali walio ahidiwa.
Rudi kwenye Sura

202. Itawateremkia adhabu kwa ghafla bila ya kuitaraji, wala wao hawajui kama inakuja.
Rudi kwenye Sura

203. Watasema itapo teremka hiyo adhabu: Je, tutapewa muhula? Haya ni kwa majuto kwa kupitiwa na Imani na kutaka waakhirishiwe adhabu. Lakini hawajibiwi.
Rudi kwenye Sura

204. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watu wa Makka wameghurika na kuchelewesha kwangu kuwaadhibu, basi ndio wanaihimiza? Anakusudia  Subhanahu Aliye takasika kuzisafihi akili zao kwa sababu ya kuhimiza kwao adhabu juu ya kuwaonya na kuwatisha.
Rudi kwenye Sura

205. Je, umefikiri ukajua, kama Sisi tuliwastarehesha  kwa uhai kwa muda wa miaka mingi pamoja na maisha mema?
Rudi kwenye Sura

206. Kisha ikawateremkia adhabu iliyo ahidiwa.
Rudi kwenye Sura

207. Kustarehe kwao kwa umri mrefu na maisha mema hakutowakinga hata chembe na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwani adhabu ya Mwenyezi Mungu itakuja tu, kama si leo kesho. Wala hapana kheri katika neema ambayo khatima yake ni adhabu.
Rudi kwenye Sura

208. Na mwendo wetu kwa kaumu zote ni kuwa hatuuteketezi umma ila baada ya kuwatumia Mitume wa kuwaonya kwa kufuata hoja,
Rudi kwenye Sura

209. Wakumbuke na wazingatie. Wala si shani yetu kudhulumu hata tuuadhibu umma kabla ya kuwaletea Mtume.
Rudi kwenye Sura

210. Qur'ani inakataa waliyo yasema makafiri wa Makka ya kwamba Muhammad anafuata majini, nao  ndio wanampa Qur'ani. Qur'ani inasema: Mashetani hawakuiteremsha hii Qur'ani.
Rudi kwenye Sura

211. Wala haiwafalii wao kuiteremsha, na hawawezi kufanya hivyo.
Rudi kwenye Sura

212. Kwani hao hakika wanazuiwa wasiisikie Qur'ani pale inapo funuliwa kwa Muhammad s.a.w.
Rudi kwenye Sura

213. Basi wewe muelekee Mwenyezi Mungu ukiendelea na usafi wako wa ibada, wala usishughulike na fisadi za madai ya washirikina na mwendo wao muovu. Na hivi kutakiwa Mtume s.a.w. awe na ikhlasi ya namna hii ni wito kwa jamii ya watu waliomo katika umma wake.
Rudi kwenye Sura

214. Watie khofu ya adhabu ya shirki na maasi walio karibu nawe katika jamaa zako.
Rudi kwenye Sura

215. Na kuwa mpole kwa wanao itikia wito wako wa Imani.
Rudi kwenye Sura

216. Pindi wakikuasi na wasikufuate basi jitenge nao, na jitenge na vitendo vyao vya ushirikina na maasi yote.
Rudi kwenye Sura

217. Na tegemeza mambo yako kwa Mwenye nguvu, Mwenye uweza wa kuwatenda nguvu adui zako kwa utukufu wake, na kukunusuru wewe na kumnusuru kila mwenye kufanya a'mali yake kwa usafi wa niya.
Rudi kwenye Sura

218. Ambaye anakuona pale unapo simama kwa ibada za usiku na vitendo vyote vya kheri.
Rudi kwenye Sura

219. Na anaona mwendo wako kati ya wanao sali, kwa kusimama, na kukaa, na kurukuu na kusujudu, pale unapo waongoza katika Sala.
Rudi kwenye Sura

220. Hakika Yeye Subhanahu ndiye Mwenye kusikia dua zako na dhikri zako, ndiye Mjuzi wa kujua niya yako na vitendo vyako. Ni kama kwamba Subhanahu anamwambia: Usichukue taklifu kubwa bila ya kiasi katika mashaka ya ibada, kwani uyatendayo yote nayaona na nayasikia Mimi.
Rudi kwenye Sura

221. Washirikina walisema: Mashetani ndio wanamsomea Qur'ani Muhammad. Qur'ani ikawajibu: Nikupeni khabari watu gani Mashetani ndio wanawateremkia, na wakawashawishi?
Rudi kwenye Sura

222. Wanamteremkia kila mwenye kubeba dhambi za namna mbaya kabisa za uwongo, na madhambi ya kuchusha kabisa. Nao ni hao makohani mafisadi ambao tabia zao na tabia za Mashetani ni jinsi moja na zimewafikiana.
Rudi kwenye Sura

223. Hao hutega masikio yao kwa Mashetani, na kwao wakapata mambo ya dhana dhana tu. Na wengi wao ni waongo, na huzidisha tena juu ya kauli walizo zipata kwa Mashetani.
Rudi kwenye Sura

224. Makafiri wanasema: Hii Qur'ani ni mashairi, na Muhammad ni mtungaji mashairi. Mwenyezi Mungu ameyavunja haya kwa kuthibitisha kuwa hakika Qur'ani imejaa hikima na hukumu. Mpango wake unapingana na mpango wa mashairi ambao unategemea juu ya kweli na uwongo. Na amebainisha kwamba hali ya Muhammad s.a.w. inapingana na hali ya watungaji mashairi. Yeye anasema kwa hikima, wao wanasema kwa udanganyifu. Na hii ndiyo hali ya wengi katika watungaji mashairi.
Rudi kwenye Sura

225. Kwani huwaoni vile wanavyo tangatanga katika mabonde ya maneno wala hawaongoki kwenye Haki?
Rudi kwenye Sura

226. Na kwamba wao husema kwa ndimi zao wasio yaambatisha na vitendo vyao?
Rudi kwenye Sura

227. Lakini walio hidika kwa hidaya ya Mwenyezi Mungu, na wakatenda mema mpaka zikatua katika nafsi zao sifa bora, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi mpaka ikathibiti khofu katika nyoyo zao, hawa basi huyafanya mashairi kama dawa ilio sibu kwa ugonjwa wake. Na hupambana kwa ajili ya kuiwania Dini yao na kusimamisha Haki, inapo kuwa Haki inafanyiwa jeuri. Na walio dhulumu nafsi zao kwa shirki na kumkejeli Mtume kwa mashairi, watatafuta wapi pa kuikimbia shari na hilaki wanayo iendea.
Rudi kwenye Sura