1. Itakapo pasuka mbingu,

Rudi kwenye Sura

2. Na nyota zitakapo pukutika na kutawanyika,

Rudi kwenye Sura

3. Na bahari zikafurika na kuingiliana kwa kuondoka viziwizi baina yao,

Rudi kwenye Sura

4. Na makaburi yakafunuliwa na wakatoka maiti walio kuwamo,

Rudi kwenye Sura

5. Hapo basi kila nafsi itajua nini kheri au shari iliyo tanguliza na iliyo chelewesha.

Rudi kwenye Sura

6. Ewe mwanaadamu! Kitu gani kilicho kukhadaa wewe na Mola wako Mlezi Mtukufu hata ukafanya jeuri ya kwenda kumuasi? (Ni dhaahiri kuwa Sayyid Abdulla bin Ali bin Nassir aliye tunga utenzi wa Kiswahili maarufu uitwao Al Inkishaf aliiwaza Aya hii alipo tunga ubeti huu:
                 Moyo wangu nini huzundukani
                 Likughurielo hela ni nni?
                 Hunelezi nami kalibaini
                 Liwapo na sura nisikataye )

Rudi kwenye Sura

7. Mungu wako huyo ndiye  aliye kuumba nawe hukuwa chochote, akakuumba na viungo vya kukuletea manufaa, akakufanya umenyooka kwa umbo sawa sawa.

Rudi kwenye Sura

8. Akakujenga na akakuleta katika sura yoyote aliyo itaka.

Rudi kwenye Sura

9. Hamwachi? Bali nyinyi mnakadhibisha malipo ya Siku ya Kiyama!

Rudi kwenye Sura

10,11,12. Na hakika wapo juu yenu Malaika walinzi, ambao ni waheshimiwa kwetu, wanasajili vitendo vyenu vyote mvitendavyo, vya kheri na shari.

Rudi kwenye Sura

13. Hakika wale walio ni wa kweli katika Imani yao wapo katika neema kubwa.

Rudi kwenye Sura

14,15. Na hakika walio iacha amri ya Mwenyezi bila ya shaka watakuwa katika Moto unao unguza, wataingia humo Siku ya Malipo.

Rudi kwenye Sura

16. Na wala hawatatoka katika Jahannamu!

Rudi kwenye Sura

17. Na nini kitakujuvya ni nini hiyo Siku ya Malipo, na mambo yake yamepindukia ujuzi wako na fikra zako?

Rudi kwenye Sura

18. Tena ni nini kitacho kujuvya ni nini hiyo Siku ya Malipo kwa vitisho vyake na shida zake?

Rudi kwenye Sura

19. Siku ambayo nafsi haitakuwa na mamlaka yoyote juu ya nafsi ya kuifaa au kuidhuru; na amri yote siku hiyo itakuwa ni ya Mwenyezi Mungu peke yake!

Rudi kwenye Sura