1. Naapa kwa mbingu na nyota inayo tokeza usiku!

Rudi kwenye Sura

2,3. Na kitu gani kitakujuvya ukweli wa nyota hii? Ni hiyo inayotoa mwanga wake katika giza.

Rudi kwenye Sura

4. Hapana nafsi ila inayo mlinzi wa kuiangalia na kudhibiti vitendo vyake.

Rudi kwenye Sura

5. Basi naafikiri mtu, yeye kaumbwa kutokana na nini?

Rudi kwenye Sura

6. Ameumbwa mtu kutokana na maji yanayo toka kwa nguvu.

Rudi kwenye Sura

7. Maji haya yanatoka baina ya uti wa mgongo na mbavu za mwanamume na mwanamke.
 S'ULB ni sehemu za uti wa mgongo; na TARAAIB ni mafupa ya vifua, yaani mbavu. Masomo ya watoto wanapo kuwa ndani ya matumbo ya mama zao (Embryology). yamedhihirisha kuwa viini vya vyombo vya uzazi na mkojo katika mtoto ndani ya tumbo la mama yake vinadhihiri baina ya khalaya (cells) za mishipa itakayo kuwa mafupa ya uti wa mgongo, na baina ya khalaya zitakazo kuwa mafupa ya kifua.
Mafigo hubakia pahala pake, na kokwa huteremka kwenye pahala pake pa kawaida katika pumbu wakati wa kuzaliwa. Na juu ya kuteremka kokwa chini mishipa inayo inywesha damu maisha yake yote inatokana na mishipa ya mafigo.
Hali kadhaalika mishipa ya Navo inayo peleka kuhisi na ikasaidia kuzalisha vitu vya uhai na yaliyo khusiana na hayo kama maji yanayo toka kwenye mshipa wa kifua wa kumi unao tokana na ubongo wa uti wa mgongo kwenye kipingili cha kumi na kumi na moja.
Yaliyo wazi kutokana na hayo ni kwamba vyombo vya uzazi na vinavyo lisha vyombo hivyo, na vyombo vya damu, vipo katika kiwiliwili baina ya uti wa mgongo na mbavu.

Rudi kwenye Sura

8. Hakika Mwenyezi Mungu aliye muumba hivi hapo mwanzo, bila ya shaka ni Muweza wa kumuumba tena baada ya kufa kwake.

Rudi kwenye Sura

9. Siku dhamiri zitapo fanyiwa mtihani, na zitengwe mbali mbali baina ya ziliyo kuwa nzuri na ziliyo kuwa mbovu.

Rudi kwenye Sura

10. Basi hapana mtu wakati huo ataye kuwa na nguvu ya kujikinga nafsi yake, wala hatakuwa na msaidizi wa kumnusuru.

Rudi kwenye Sura

11. Naapa kwa mbingu yenye mvua inayo rejea na kuja mara kwa mara!

Rudi kwenye Sura

12. Na ardhi inayo pasuka kwa kuchipuka mimea!

Rudi kwenye Sura

13,14. Hakika hii Qur'ani ni yenye kupambanua baina ya kweli na uwongo. Wala haina nuksani yoyote ya mchezo au maskhara.

Rudi kwenye Sura

15. Hakika hao wanao ikadhibisha Qur'ani wanaipangia njama kutaka kuiharibia, njama zenye kufikia ukomo!

Rudi kwenye Sura

16. Lakini Mimi nitawalipa, na nitavipambanisha hivyo vitimbi vyao kwa vitimbi madhubuti ambavyo hawataweza kujikinga navyo.

Rudi kwenye Sura

17. Basi wangojee hao makafiri! Wape muhula wa karibu mpaka nikuamrishe amri gani kali ya kuwatendea.

Rudi kwenye Sura