1. Litakase jina la Mola wako Mlezi lilio tukufu na kila kitu kisicho kuwa kinaelekeana nalo.

Rudi kwenye Sura

2. Aliye umba kila kitu, na akajaalia uumbaji wote sawa sawa katika hukumu na kupangana.

Rudi kwenye Sura

3. Na akakadiria kwa kila kitu kwa mujibu wa maslaha yake, na akakiongoza.

Rudi kwenye Sura

4. Na ambaye akatoa kwenye ardhi mimea namna mbali mbali ya kuwalisha wanyama.

Rudi kwenye Sura

5. Na akaifanya mimea hiyo baada ya kuwa kijani imestawi, ikakauka na imekuwa myeusi!

Rudi kwenye Sura

6. Ewe Muhammad! Sisi tutakujaalia uwe ni mwenye kuisoma Qur'ani kwa ufunuo kutoka kwetu, na wala hutosahau utacho kihifadhi.

Rudi kwenye Sura

7. Isipo kuwa anacho taka Mwenyezi Mungu ukisahau, kwani hakika Yeye Mtukufu anayajua wanayo yadhihirisha waja wake na wanayo yaficha, ikiwa maneno au vitendo.

Rudi kwenye Sura

8. Na tutakuwezesha kupita njia ya kufikilia kwa wepesi mambo yako yote.

Rudi kwenye Sura

9. Basi wakumbushe watu ikiwa kukumbusha kutaleta manufaa, kwani inavyo faa ndio kuwanafiisha.

Rudi kwenye Sura

10. Watanafiika kwa ukumbusho wako wanao mwogopa Mwenyezi Mungu.

Rudi kwenye Sura

11. Na atajitenga na ukumbusho mpotovu anaye shikilia kufanya inda na ukafiri.

Rudi kwenye Sura

12. Ambaye ataingia kwenye Moto mkubwa ulio andaliwa kuwa ndio malipo yake.

Rudi kwenye Sura

13. Tena hatokufa huko Motoni akapumzika kwa kifo, wala hawi hai kwa uhai wa kustarehe nao.

Rudi kwenye Sura

14. Hakika amefuzu mwenye kujisafisha na ukafiri na maasi.

Rudi kwenye Sura

15. Na akalikumbuka jina la Muumba wake kwa moyo wake na ulimi wake, na akasali kwa unyenyekevu kama itakikanavyo.

Rudi kwenye Sura

16. Bali nyinyi hamfanyi hayo yanayo pelekea kufanikiwa, lakini katika hima zenu mnatanguliza maisha ya duniani kuliko ya Akhera.

Rudi kwenye Sura

17. Na Akhera ni bora kuliko dunia, kwa usafi wa neema zake, na ni yenye kubaki na kudumu zaidi.

Rudi kwenye Sura

18,19. Hakika haya yote yaliyo tajwa katika Sura hii bila ya shaka yamethibitishwa katika Vitabu vya zamani, Vitabu vya Ibrahimu na Musa; kwani haya yamewafikiana na mafunzo ya dini zote na yamesajiliwa katika Vitabu vya mbinguni.

Rudi kwenye Sura