1. Naapa kwa wakati wa kupanda juu jua, na ni wakati wa uchangamfu na kazi!

Rudi kwenye Sura

2. Na naapa kwa usiku unapo tulia na ukatanda kote kiza chake!

Rudi kwenye Sura

3. Ewe Muhammad! Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukuchukia.

Rudi kwenye Sura

4. Na matokeo ya mambo yako, mwisho wake, yatakuwa bora kuliko mwanzo wake.

Rudi kwenye Sura

5. Na ninaapa kuwa bila ya shaka hapo Mola wako Mlezi atakupa kheri za duniani na Akhera hata utaridhia.

Rudi kwenye Sura

6. Kwani hakukukuta wewe yatima unahitaji wa kukutunza naye akakupa makaazi ya kukuhifadhi kwa mwenye kukuangalia vyema kwa mambo yako?

Rudi kwenye Sura

7. Na akakuona umebabaika hukukinaika na itikadi zilizo kuzunguka, naye akakuongoa kwenye Njia ya Haki?

Rudi kwenye Sura

8. Akakukuta fakiri wa mali naye akakutajirisha kwa kukupa riziki?

Rudi kwenye Sura

9,10,11. Ikiwa hii ndiyo hali yetu nawe, basi yatima usimdhili, na mwenye kuomba au kuuliza usimjibu kwa ukavu, na ama neema za Mola wako Mlezi zitangaze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa ndio kudhihirisha neema.

Rudi kwenye Sura