1. Hakika tumekukunjulia kifua chako kwa kuwa tulitia ndani yake Uwongofu na Imani.

Rudi kwenye Sura

2. Na tumekupunguzia mizigo iliyo kuwa mizito juu ya mgongo wako, kwa kukuunga mkono na kukusahilishia mambo yako,

Rudi kwenye Sura

3. Ambayo yalikuwa ni mazito juu ya mgongo wako.

Rudi kwenye Sura

4. Na tumelitukuza jina lako, tukalifanya linatajwa na ulimi wa kila Muumini pamoja na jina letu.

Rudi kwenye Sura

5. Hizo ni baadhi ya neema zetu juu yako. Basi kuwa na yakini na uweza wa Mwenyezi Mtukufu, kwani pamoja na uzito upo wepesi mwingi unao kuja nao.

Rudi kwenye Sura

6. Hakika pamoja na uzito (wakati huo huo ijapo kuwa wewe hujui), upo wepesi mwingi vile vile.

Rudi kwenye Sura

7. Basi ukipata nafasi katika kazi ya kuwalingania watu, na mambo yaliyo khusiana na Jihadi, endelea na jitihada ya ibada na jishughulishe nafsi yako katika hayo.

Rudi kwenye Sura

8. Kwa Mola wako Mlezi tu ndio uelekee kwa kumwomba na kumhitajia.

Rudi kwenye Sura