mecca_1.jpgFIQHI ILIYOWEPESISHWA: Tunza

Farouk Abdalla Al-Barwani

Tunza

Tunamuomba Mola wetu Mlezi, s.w.t. atujaaliye haya aliotujaalia kuyatenda na yote mengineyo yawe ni ya kheri yenye wingi wa barka, na yawe ni kwa ajili yake Yeye Pekee. Na kwa Rehma Zake zilizoeneakila upande, tunamuomba Subhaanahu wa Ta'aala atuongezeehasanaati kwenye mizani za wazee wetu, waliotangulia mbele ya Haqina waliohai; na katika mizani zetu, na mizani za jamii ya Waumini, Amin, Yaa Rabbi, Amin. Tunamuomba vilevile Mola wetu Mlezi s.w.t.haya aliotujaalia kuyafanya yapate kusomwa, yafahamike na yatumikekwa manufaa ya jamii ya Waumini. Tumefanya haya, si kwa kuwa niwenye ujuzi katika elimu hii, wala kuwa tuna ujuzi wa yoyote kati yalugha mbili hizi, hatuna ujuzi laa wa lugha ya Kiarabu, walaa wa lugha yaKiswahili; bali tumeona ni wajib wetu kuutekeleza waajibuu huu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awajazei kheri kila aliesaidia mpaka kitabu hiki kikatoka na kufika mikononi mwa ndugu zetu. Vilevile tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atughufirie makosa yetu na makosa yaliyomo kwenye haya tuliyoyatarjimu. Kwa ndugu zetu, tunawaomba na wao watusamehe kwa kila kosa liliyomo kwenye tarjuma hii, hapana shaka yamo makosa, kwani kukamilika na kutokuwa na kukosa; ni kwake Yeye Subhaanahu wa Ta'aala Pekee. Mola wetu Mlezi Yeye ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu.

 

Kitabu Hiki

Asili ya kitabu hiki, kina juzuu mbili; juzuu ya kwanza ina khusu 'ibaadaat, Sala, Saumu, Zaka na Hijja. Juzuu ya pili ina khusu mu'amalaat, yaani maingiliano baina ya waja, ndoa na 'talaqa, kuuza na kununua, kukopa na kukopesha, wasia, na mengineo ya makhusiano baina ya waja. Hii tarjuma tuliojaaliwa kuifanya ni ya juzuu ya kwanza, yaani yenye kuhusu 'ibaadaat Penye majaaliwa, Inshaallah tutafanya tarjuma ya juzuu ya pili; yaani, yenye kukhusu mu'amalaat. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujaalie tawfiq na uwezo tutekeleze azma hii kwa karibuni, Inshaallah.

 

Khitilafu za Rai za Wanazuoni ni Rehma

Kukhitalifiana rai Wanazuoni (Wanazuoni walio kubalika ilimu yao na uchaungu wao), katika, yaani matawi ya Sharia, si kukhitalifiana katika, yaani msingi ya Sharia; ni rehma kwa Umma. Kutokana na msingi huu, na vile kuwa hakika ni kwamba vitabu viwili hivi, yaani "Fiqh Sunna" na "Fiqh Iliyowepesishwa" ni vimoja; kwani machimbuko yake ni mamoja, bali hii "Fiqh Iliyowepesishwa", mengi yake ni mukhtasari wa yale yaliyomo kwenye "Fiqh Sunna".

Katika kufanya hivyo, tumechukua sehemu ya: "Yenye Kutengua Udhu", sehemu ile ambayo kwenye "Fiqh Iliyowepesishwa" haikutajwa. Vilevile tumeeleza kukhusu kusali (kwa dharura) bila ya kutia udhu walaa kutayammam. Pia tumeeleza kukhusu "Sunna ya Kabla

Sala ya Alfajiri", vilevile hii ni sehemu ambayo haikuelezwa kwenye "Fiqh Iliyowepesishwa".

Vitabu viwili hivi vyote vinakubalika na kutumika katika ulimwengu wa Kiislam.

Upokezi wa Hadithi (Zilizomo Humu) Katika upokezi wa Hadithi za Mtume wetu Mpenzi s.a.w. Inaposemwa: "Al Sheikhan", inakusudiwa ni Al Bukhary na Muslim r.a. Inaposemwa: "Al Khamsa", inakusudiwa ni Al Bukhary, Muslim, Abu Daud, Al Nissaai, na Ibnu Maajah r.a. Inaposemwa) "Mutafaq 'Alaih", inakusudiwa kuwa hio Hadithi wamekubaliana nayo wapokezi mashuhuri wote wa Hadithi.

 


_____________________________________________________

Haki za Uchapishaji zimehifadhiwa na Mtungaji

Farouk Abdalla Al-Barwani, P.O. Box 828, Ruwi, P.C.112 Sultanate of Oman

e-mail: umojabaraka@yahoo.co.uk