1. Hizi ni Aya za Kitabu cha kusomwa, chenye kubainisha,
chenye kuweke wazi.
Rudi kwenye Sura
2. Watapenda, na watatamani sana makafiri wanao zikanya Aya za Mwenyezi
Mungu Subhanahu wa Taa'la, watapo ona adhabu ya Siku ya Kiyama, lau kuwa
walisilimu walipo kuwapo duniani, na wakafuata kwa ikhlasi Dini ya Mwenyezi
Mungu.
Rudi kwenye Sura
3. Lakini sasa wamo katika kughafilika, hawazingatii adhabu itakayo
wapata Akhera! Basi ukisha wafikishia ujumbe wako, na ukawaonya, waachilie
mbali. Wao hawana hamu ila kula, na kustarehe kwa ladha za dunia.
Tamaa ya uwongo inawazuga. Na hakika bila ya shaka yoyote watakuja jua
yatakayo wapata pale watapo yaona kwa macho yao Siku ya Kiyama.
Rudi kwenye Sura
4. Na ikiwa wao wanataka wateremshiwe adhabu ya duniani, kama Mwenyezi
Mungu alivyo wateketeza walio kuwa kabla yao, basi wajue kuwa Mwenyezi
Mungu hauteketezi mji wowote ila kwa wakati wake maalumu.
Rudi kwenye Sura
5. Hawatangulii wala hawataakhari.
Rudi kwenye Sura
6. Na uovu wa hali yao na wingi wa kughafilika kwao hata imefika
hadi kumuita Nabii wao kwa kejeli wakisema: Ewe uliye teremshiwa Kitabu
cha kukumbusha! Hapana shaka kuwa wewe una wazimu moja kwa moja!
Huko kumuita kuwa ndiye aliye teremshiwa Ukumbusho, yaani Mawaidha, hakukuwa
ila ni kwa kejeli tu, kumfanyia maskhara.
Rudi kwenye Sura
7. Na hadi ya ukafiri wao walizidisha juu ya matusi hayo na kejeli
kwa kusema: Laiti badala ya hicho Kitabu kilicho teremshwa ungeli tuletea
Malaika wakawa ndio hoja yenyewe, kama wewe ni msema kweli miongoni mwa
wenye kusema kweli!
Rudi kwenye Sura
8. Na Mwenyezi Mungu aliye tukuka neno lake aliwajibu: Sisi hatuwateremshi
Malaika ila huwa pamoja nao Haki ya nguvu yenye kuthibiti ambayo haina
njia ya kuikataa. Basi wakiikanya huwa tena hawapewi muhula wowote, bali
huteremshiwa adhabu ya hapa hapa duniani hapo hapo!
Rudi kwenye Sura
9. Na hakika, kwa ajili ya kuwa Wito wa Nabii huyu kwendea Haki udumu
mpaka Siku ya Kiyama, hatuwateremshi Malaika, bali tumewateremshia hii
Qur'ani ambayo kukumbusha kwake kunaendelea daima dawamu. Na Sisi
ndio wenye kuilinda isiingiliwe na mageuzo na mabadiliko yoyote mpaka kusimama
Kiyama.
Rudi kwenye Sura
10. Na ewe Mtume Muaminifu! Usihuzunike; kwani Sisi tuliwatuma Mitume
kabla yako kwa mataifa ambao wameshikilia upotovu kama hao walivyo shikilia.
Na wao wamepita pamoja na wa kale walio teketezwa kwa ukafiri wao!
Rudi kwenye Sura
11. Wala mtindo wao hao walio watangulia kwa kushikilia upotovu haukuwa
ila kuwafanyia maskhara Mitume wao, Mtume baada ya Mtume, kama wanavyo
kufanyia kejeli wewe! Huo ndio mtindo wa wapotovu!
Rudi kwenye Sura
12. Kama tulivyo itia Qur'ani katika nyoyo za Waumini ikaingiza mwangaza,
basi kadhaalika tumeingiza upotovu katika nyoyo za walio pigwa muhuri wa
ukosefu; hali ya katika nyoyo zao ikawa kinyume cha hayo. Upotovu ukatia
mizizi katika roho zao.
Rudi kwenye Sura
13. Wakhalifu hao hawaamini. Na mwendo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu
kuwapa muhula mpaka waione adhabu chungu ya Siku ya Kiyama ndio kama ulivyo
kwisha tangulia.
Rudi kwenye Sura
14. Watu hao wanataka wateremshiwe Malaika. Ewe Nabii! Usidhani kuwa
ndio wataamini wakiteremshiwa. Bali hata tungeli wafungulia mlango wa mbingu
wakawa wanapanda huko wakaona maajabu yaliyoko, na wakawaona Malaika,
Rudi kwenye Sura
15. Bado wasingeli amini, na wangesema: Macho yetu yamefumbwa tusione,
na yamefunikwa. Bali hayo si lolote ila ni uchawi tu, tumerogwa! Basi hapana
faida ya ishara yoyote maadamu nyoyo zao zimeenea ukafiri.
Rudi kwenye Sura
16. Na Sisi tumeweka mbinguni sayari na nyota, kwa makundi yenye
hisabu zake na yenye kukhitalifiana umbo lake na sura yake. Na kadhaalika
tukazipamba kwa wenye kuziangalia kwa kutuza na kuzingatia, na kuchunguza
kwazo dalili za uwezo wa Muumbaji wao.
Rudi kwenye Sura
17. Lakini Sisi tumezihifadhi na kila shetani anaye stahiki kupigwa
vimondo na kufukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Rudi kwenye Sura
18. Na yeyote katika hao mashetani wanao jaribu kuibia kusikiliza
maneno yanayo jiri baina ya wakaazi wa hizi nyote, basi Sisi tunampopoa
kwa vijinga vya moto vya mbinguni vinavyo onekana wazi.
Rudi kwenye Sura
19. Na tumekuumbieni ardhi, na tumekutengenezeeni mpaka ikawa kama
busati lilio tandikwa, na tukaweka ndani yake milima iliyo simama imara.
Na tumekuotesheeni ndani namna mbali mbali za mimea ya kukufaeni kwa uhai
wenu, na tumeifanya kwa vipimo na zama maalumu katika kukua kwake, na faida
yake kwa kula, na kwa kadiri ya haja zenu na kwa vipimo vyake, na sura
yake kwa umbo na tabia.
Aya hii inaeleza uhakika wa uumbaji ambao haukujuulikana ila katika
zama za hivi karibuni. Nayo ni kuwa kila kabila ya mimea imefanana kati
yao kwa kuonekana na undani wake, hata katika sehemu zake ndogo ndogo,
katika viungo vyake vyote vya hiyo mimea. Na hali kadhaalika katika "Khalaya"
au "Cells" za hiyo mimea ya kabila fulani, kwa ajili ya kutimiza kazi iliyo
kusudiwa kiungo hicho cha mmea. Na pia sehemu za mimea ya hizo kabila zao
na vilivyo undwa katika viungo vyake utaona mnasaba wake umethibiti
kila mwaka, ukilinganisha kwa wakati ule ule katika miaka mingine
Rudi kwenye Sura
20. Na tumekujaalieni katika ardhi sababu za maisha mema. Kwani
ndani yake yamo mawe ya kujengea majumba, na wanyama mnao nafiika kwa nyama
yao, au ngozi zao, au manyoa yao. Na yapo maadeni yanayo toka chini ya
ardhi, na mengineyo. Kama ilivyo kuwa humo zipo sababu za kukuleteeni nyinyi
maisha mema, basi humo pia wanapata maisha wenginewe ambao wapo chini ya
mamlaka yenu, kama watoto na wafwasi, ambao Mwenyezi Mungu pekee ndiye
anaye waruzuku wao na nyinyi.
Rudi kwenye Sura
21. Na hapana chochote cha kheri ila kiko kwetu kama mahodhi yaliyo
jaa, nasi tunakiweka tayari na tunakitoa kwa wakati wake. Na hatuwateremshii
waja wetu ila kwa kiasi maalumu, kwa mujibu tunavyo pima kwa hikima yetu
ya maumbile.
Rudi kwenye Sura
22. Na Sisi tulipeleka pepo zilizo beba mvua na zilizo beba mbegu
za mimea, na tukateremsha maji ya kukunywesheni. Na hayo ni kwa kufuata
vile tutakavyo. Na yeyote yule hawezi kuyatenda kama hayo ila awe nayo
kwake kama mahodhi au mabirika.
Aya hii imeitangulia sayansi kwa kusema kuwa upepo unafanya kazi
kubwa katika kubeba pollen, chembe dume za kupandishia mimea, kupelekea
sehemu za uke za mimea mingine, na kwa hivyo yakazalikana mazao. Na pia
haikujuulikana ila mwanzo wa karne hii tuliyo nayo kwamba upepo unazalisha
mawingu yanayo nyesha mvua. Kwani "Nucleons" ambazo juu yake hujumuika
sehemu za mvuke wa maji na zikawa chembe chembe za maji ndani ya wingu,
ndizo chanzo cha mvua inayo chukuliwa na pepo kupelekwa kwenye majimbo
yanayo fikiwa na mawingu. Misingi ya hizo "Nucleons" ni chumvi ya bahari,
na vinavyo chukuliwa na upepo juu ya uso wa ardhi, na "Oxides" na vumbi
vumbi, n.k. Na vyote hivyo ni lazima kwa ajili ya mvua.
"Wala si nyinyi mnayo yaweka". Imethibiti kwa sayansi ya kisasa
kuwa mvua inaanza kwa mvuke kutokana na uso wa ardhi na bahari, kisha inarejea
hali ile ile tena kama ilivyo tajwa. Ikinya mvua hunywesha kila kilicho
na uhai katika ardhi, na huinywesha ardhi yenyewe. Wala haiwezekani kuzuilika,
kwa sababu ikichuruzika kutokana na vyote vyenye uhai na katika ardhi ikaingia
baharini, tena kisha huanza kuzunguka mara ya pili kwa kupanda mvuke kutoka
baharini. Basi hali ni hivyo mzunguko. Hapa ndio inabainika maana ya Aya
"Wala si nyinyi mnayo yaweka."
Rudi kwenye Sura
23. Na ni Sisi tu peke yetu ndio tunavipa vitu vyote uhai, kisha
tunavipelekea mauti, kwani uumbaji wote ni wetu.
Rudi kwenye Sura
24. Na kila mmoja wenu ana muda wake alio pimiwa. Sisi ndio tunao
ujua. Tunawajua walio tangulia kwa kufa na kuwa hai, na pia wanao taakhari.
Rudi kwenye Sura
25. Na hakika walio tangulia na walio taakhari watakusanywa wakati
mmoja. Na Mwenyezi Mungu atawahisabia na atawalipa. Na hayo ni kwa mujibu
wa hikima yake na ujuzi wake. Na Yeye ndiye anaye itwa Mwenye hikima, Mwenye
ujuzi.
Rudi kwenye Sura
26. Na Sisi katika kuumba kwetu walimwengu katika dunia hii, tumeumba
namna mbili - Tumemuumba mtu kwa udongo mkavu wenye kutoa sauti ukigongwa.
Rudi kwenye Sura
27. Na makhaluku wengine ni majini, ambao tuliwaumba mbele, alipo
umbwa asili yake Iblisi kutokana na moto mkali mno unao toka katika tundu
za mwili wa mtu.
Rudi kwenye Sura
28. Ewe Nabii! Kumbuka asli ya viumbe. Pale alipo sema Aliye kuumba,
Mola Mlezi wa viumbe vyote, kuwaambia Malaika: Mimi nataka kumuanzisha
mtu niliye muumba kutokana na udongo mkavu, wenye kutoa sauti ukigongwa,
nao umebadilika rangi, na una sura.
Rudi kwenye Sura
29. Nikisha kamilisha kumuumba, na nikampulizia roho ambayo ninaimiliki,
basi teremkeni kwa nyuso zenu mkimsujudia, kwa kumwamkia na kumhishimu.
Rudi kwenye Sura
30. Wakasujudu wote kwa kuit'ii amri ya Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye Sura
31. Lakini Iblisi alijivuna na akakataa kuwa pamoja na Malaika waliyo
it'ii amri ya Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye Sura
32. Hapo basi Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Ewe Iblisi! Kitu gani
kilicho kupelekea hata ukaasi na usiwe pamoja na wanyenyekevu walio sujudu?
Rudi kwenye Sura
33. Iblisi akasema: Si shani yangu mimi kumsujudia mtu uliye muumba
kwa udongo mkavu, wenye kutoa sauti ukigongwa, nao umegeuka rangi, wenye
kutiwa sura.
Rudi kwenye Sura
34. Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Ukiwa wewe umekuwa a'asi, umetokana
na ut'iifu wangu, basi tokelea mbali kwenye Bustani hii! Kwani hakika wewe
umefukuzwa kwenye rehema yangu na pahala pa hishima.
Rudi kwenye Sura
35. Na Mimi nimekwisha kuhukumia ubaidike na rehema na utukufu mpaka
Siku ya Kiyama, Siku ya Hisabu na Malipo. Na hapo ndipo utapo pata adhabu,
wewe na wanao kufuata .
Rudi kwenye Sura
36. Iblisi akasema, hali naye kesha kuwa ni mwenye kumuasi Mwenyezi
Mungu: Ewe Muumba wangu! Nipe muhula, nibakishe usinitwae mpaka Siku ya
Kiyama, Siku watapo fufuliwa watu wakawa hai baada ya kufa kwao.
Rudi kwenye Sura
37. Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Wewe utabakishwa, umepewa muhula,
Rudi kwenye Sura
38. Mpaka wakati niliyo ukadiria, ninao ujua Mimi. Na kama utavyo
kuwa mrefu una kikomo.
Rudi kwenye Sura
39. Akasema Iblisi, mkhalifu, a'asi: Ewe Muumba wangu unaye nibakisha!
Umenitakia upotofu, nami nikatumbukia ndani yake. Basi kwa sababu hiyo
nahakikisha kuwa nitawapambia wanaadamu maovu wayaone mazuri, na nitafanya
kila juhudi kuwapotoa wote!
Rudi kwenye Sura
40. Wala hawatoepukana na upotovu wangu ila wale waja wako walio
kufanyia ikhlasi Wewe na nisio weza kuzimiliki nyoyo zao kwa zilivyo kuwa
imara kwa kukumbuka Wewe.
Rudi kwenye Sura
41. Hakika usafi wa waja walio isafia niya Dini yao ndio Njia Iliyo
Nyooka, na haki yangu nisiikiuke, kwani hao siwezi kuwapotoa. (Tafsiri
hii yaonyesha maneno hayo ni ya Iblisi. Lakini Tafsiri nyengine zinasema
maneno hayo ni ya Mwenyezi Mungu, kwa mfano ya Abdulla Saleh, Abdulla Yusuf,
Pickthall, Razi, Baidhawi, Qurtubi, Zamakhshari, Ibn Kathir, Assad.)
Rudi kwenye Sura
42. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Hakika waja
wangu walio nisafia Mimi Dini yao wewe huna uwezo wa kuwapoteza.
Lakini wapotovu, walio zama katika upotovu, walio kufuata wewe, basi hao
ndio unayo madaraka juu ya nyoyo zao.
Rudi kwenye Sura
43. Na hakika Moto mkali mno ndio wameahidiwa hao wote kuwa
ndiyo adhabu ya kutia uchungu.
Rudi kwenye Sura
44. Wala huo Moto mkali hauna mlango mmoja tu, bali una milango saba
kwa ajili ya wingi wanao stahiki kuingia humo. Na kila mlango una kundi
lake makhsusi. Na kila kundi una cheo chake maalumu cha kulingana na uovu
wake.
Rudi kwenye Sura
45. Haya ni malipo ya wanao mfuata Shetani. Ama wale ambao
Shetani kashindwa kuwapotoa, kwa kuwa wameweka kinga baina yake na nyoyo
zao, hao watapata Mabustani yaliyo bora, na chemchem zinazo pita .
Rudi kwenye Sura
46. Mola wao Mlezi atawaambia: Ingieni katika Bustani hizi kwa utulivu
na amani. Kwani hapana khofu juu yenu, hamhuzunikii nyakati zenu.
Rudi kwenye Sura
47. Na hakika watu wa Imani wataishi katika kheri hii na nafsi zao
zimetua. Kwani tumezitoa chuki zilizo kuwamo katika nafsi hizo. Wote hao
watakuwa ndugu waketi juu ya viti vya enzi zikitazamana nyuso zao kwa furaha
na mahaba, wala hawawi mmoja nyuma ya mwenzie wakichunguliana visogoni.
Rudi kwenye Sura
48. Hawapatwi na machofu huko. Na hiyo ni neema ya daima, wala hawatotoka
humo milele.
Rudi kwenye Sura
49. Ewe Nabii muaminifu! Wape khabari waja wangu wote kwamba Mimi
ni Mwingi wa kughufiria na kusamehe kwa mwenye kutubu, akaamini, na akatenda
mema. Na kwamba Mimi ni Mwingi wa kuwarehemu.
Rudi kwenye Sura
50. Na wape khabari kwamba adhabu ninayo wateremshia wenye kuasi
na kukufuru ni adhabu yenye kutia machungu kweli, na adhabu yoyote nyengineyo
haihisabiwi kuwa ina machungu mbele ya hii.
Rudi kwenye Sura
51. Ewe Nabii! Waambie pia, katika kubainisha rehema yangu makhsusi
katika dunia na adhabu yangu kwa wenye kuasi humo, khabari ya Malaika walio
mfikia Ibrahim kama wageni.
Rudi kwenye Sura
52. Ewe Muaminifu! Watajie pale walipo ingia kwake, naye akawaogopa.
Wao wakamwambia: Amani kwako, na tulia! Yeye akasema: Sisi tunakuogopeni,
kwani mmetujia kwa ghafla, sio wakati wa dasturi wa kufika wageni, na hatujui
mna nini!
Rudi kwenye Sura
53. Wakasema: Usiogope, na tuwa moyo! Kwani tunakubashiria mwana,
ambaye Mwenyezi Mungu Mtukufu atampa siku zijazo za uhai wake ilimu
kubwa.
Inaonyesha hapa kuwa bishara hii si ya Ismail a.s. Kwani Ismail
alikuwa kesha zaliwa, naye na mama yake Haajir walikuwa wapo Makka. Bishara
hii ni ya Ibrahim na mkewe, basi kwa hivyo ni ya Is-haq mwana wa
Ibrahim na Sara.
Rudi kwenye Sura
54. Akasema: Vipi mnanibashiria mtoto na hali mimi nimekwisha patikana
na udhaifu wa ukongwe. Kwa njia gani, basi, mnanibashiria jambo hili la
ajabu?
Rudi kwenye Sura
55. Wakasema: Sisi tunakubashiria jambo lilio thibiti, ambalo halina
shaka kabisa. Basi usiwe katika wanao kata tamaa na rehema ya Mwenyezi
Mungu.
Rudi kwenye Sura
56. Ibrahim akasema: Mimi sikati tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu.
Kwani hawakati tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu ila walio potea wasio
utambua utukufu wake na uwezo wake.
Rudi kwenye Sura
57. Alivyo kuwa kaanza kuzoeana nao, alisema: Ikiwa mmenibashiria
khabari hii nzuri, je mna jambo gani jenginelo mlilo nalo baada ya haya,
enyi wajumbe mlio tumwa na Mwenyezi Mungu?
Rudi kwenye Sura
58. Wakasema hakika sisi tumetumwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa
watu walio fanya ukhalifu katika Haki ya Mwenyezi Mungu na haki ya Nabii
wao, na haki ya nafsi zao wenyewe. Ukhalifu ndio mtindo wao. Watu wenyewe
ni kaumu ya Luut'i. Basi tutawateketeza.
Rudi kwenye Sura
59. Wala hakusalimika na huo ukhalifu na adhabu yake ila ahli zake
yeye Luut'i. Basi hao Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha tuwaokoe wote.
Rudi kwenye Sura
60. Na hatoangamia katika ahli zake ila mkewe, kwani yeye hakumfuata
mumewe, bali yu pamoja na hao wakosefu ambao wanao stahiki adhabu.
Rudi kwenye Sura
61. Wale Malaika walio tumwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kuteremsha
yaliyo ahidiwa, walipo fika nchi ya Luut'i na watu wake,
Rudi kwenye Sura
62. Luut'i aliwaambia: Watu nyinyi sikujuini, na nafsi yangu inatishika
nanyi. Naogopa msituletee balaa.
Rudi kwenye Sura
63. Wakasema: Usituogope, kwani hatukukujia kwa unalo liogopa, bali
tumekujia kwa jambo la kukufurahisha, nalo ni kuwateremshia adhabu hawa
watu wako walio kukadhibisha na wakawa wanaitilia shaka hiyo adhabu au
wanaikanya.
Rudi kwenye Sura
64. Nasi tumekujia kwa amri iliyo thaabiti isiyo na shaka, nayo ni
kuiteremsha adhabu. Na kutimiza ahadi ni katika sifa yetu, kwa amri ya
Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye Sura
65. Ilivyo kuwa adhabu itawateremkia, basi wewe na ahli zako mlio
andikiwa kuokoka, tokeni baada ya kwisha ingia usiku.
Rudi kwenye Sura
66. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la alimfunulia Luut'i kwa
kumwambia: Sisi tumewahukumia na kuwakadiria wakosefu kuteketea. Watang'olewa
itapoingia asubuhi, wala hatobaki hata mmoja wao.
Rudi kwenye Sura
67. Asubuhi kulipo pambazuka waliwaona Malaika kwa sura ya binaadamu
wazuri. Wao wale wakawafurahia, wakaja ili wafanye nao vitendo vyao viovu,
vya kuwaingilia wanaume.
Rudi kwenye Sura
68. Luut'i akaogopa wasije wakatenda vitendo vyao viovu. Akasema:
Hawa ni wageni wangu, basi msinifedheheshe kwa vitendo vyenu vibaya.
Rudi kwenye Sura
69. Na mwogopeni Mwenyezi Mungu Mtukufu! Msifanye uchafu wenu, mkanipatisha
hizaya na madhila mbele yao!
Rudi kwenye Sura
70. Wale wakhalifu wakasema: Kwani si tulikukataza wewe usimkaribishe
mtu yeyote, na hivi sasa tena unatuzuia tusifanye nao tunayo yatamani?
Rudi kwenye Sura
71. Ili kuwanabihisha njia ya maumbile ya kisharia, Nabii wa Mwenyezi
Mungu Luut'i akasema: Hawa mabinti wa mji huu, nao ni binti zangu, waoeni
ikiwa mnataka kukidhi matamanio yenu.
Rudi kwenye Sura
72. Ewe Nabii Muaminifu! Naapa kwa haki ya uhai wako! Hawa wamo katika
mghafala, hawajui yatakayo wateremkia. Wamekuwa kama walio lewa! Hakika
wao wamo katika upotovu, wanatapatapa, hawajui wapite wapi.
Rudi kwenye Sura
73. Na walipo kuwa wao wamo katika ulevi wao wa mghafala nyoyo zao
na akili zao zikachotwa na ukelele mkali mno wa kutisha, wakati jua lilipo
chomoza.
Rudi kwenye Sura
74. Mwenyezi Mungu Aliye takasika katekeleza hukumu yake, akasema:
Miji yao tukaifanya juu chini kwa kuivuruga, na tukawateremshia udongo
ulio fanyika mawe ukiwateremkia kama mvua. Majumba yao yakaporomoka. Na
wakitoka nje hukuta hiyo mvua ya mawe. Kwa hivyo wakawa wamezungukwa kila
jiha.
Rudi kwenye Sura
75. Haya yaliyo washukia kaumu Luut'i ni alama wazi ya kuonyesha
vipi Mwenyezi Mungu Mtukufu anavyo timiza ahadi yake. Wajuao mambo wanayatambua
hayo, na wanayaelewa matokeo yake kwa alama zake, kwani kila kitendo chenye
sifa ya ukosefu kina alama yake isiyo potea. Matokeo yake ni mfano wa haya,
duniani na Akhera.
Rudi kwenye Sura
76. Na mabaki ya mji huu yapo yamesalia. Nayo yapo njiani katika
njia inayo pitiwa na watu. Anaye taka kuwaidhika kwayo anaweza kuwaidhika.
Rudi kwenye Sura
77. Kwa kuwa mabaki yake yapo kwenye njia iliyo wazi ni dalili ya
Mwenyezi Mungu Mtukufu kutimiza onyo lake, na Waumini wenye kut'ii Haki
wanatambua hayo.
Rudi kwenye Sura
78. Kama kaumu ya Luut'i walivyo kadhibisha, kadhaalika wakaazi wa
Kichakani kwenye msitu wenye matunda walimkanya Mtume wao. Wakawa madhaalimu
wenye kudhulumu mno katika imani yao na maingiliano yao.
Rudi kwenye Sura
79. Tukawateremshia nakama yetu. Na mabaki yao yapo njiani yanaonekana,
na mpita njia akiwa ni mtu wa Imani basi anaweza kuzingatia kwayo.
Rudi kwenye Sura
80. Na kama walio tangulia hali kadhaalika wakaazi wa Hijr walimkanusha
Mtume wao aliye tumwa kwao, na kwa hivyo wakawa wamewakanusha Mitume wote.
Kwani ujumbe wa Mwenyezi Mungu ni mmoja.
Watu wa Hijr ndio Thamud. Na Hijr ni bonde baina ya Madina na Sham.
Tazama maelezo juu ya Aya 73 ya Surat Al-Aa'raaf.
Rudi kwenye Sura
81. Tuliwabainishia hoja zenye kuonyesha uwezo wetu, na Utume wa
Mtume wetu, nao wakayapuuza, wala wasiyafikiri.
Rudi kwenye Sura
82. Nao walikuwa watu wenye nguvu na wajenzi. Walikuwa wakijenga
majumba yao katika milima na wakiichonga hiyo hiyo milima. Na wao walikuwa
wakijiamini kuwa wametua na nafsi zao na mali yao.
Rudi kwenye Sura
83. Walipo kufuru na wakakanya, zikawajia sauti za kutisha, za kuonya
kuteketea kwao, wakahiliki wakati wa asubuhi.
Rudi kwenye Sura
84. Wala mali waliyo yachuma na majumba waliyo yajenga hayakuwalinda
na hilaki iliyo wateremkia.
Rudi kwenye Sura
85. Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo kati yao katika anga, na
viliomo ndani yake, watu na wanyama, na mimea na visio na uhai, na vinginevyo
ambavyo mwanaadamu havijui, isipo kuwa kwa uadilifu, na hikima, na maslaha
ambayo hayaambatani na fisadi ya kudumu isiyo na mwisho. Na kwa hivyo basi
ni lazima siku ya kukomesha shari ifike bila ya shaka yoyote. Basi ewe
Nabii Mtukufu! Wasamehe hao washirikina adhabu ya duniani, na ingiana nao
kwa kuwastahamilia maudhi yao. Na kuwaita wito kwa hikima ni kuingiliana
kwa usamehevu na upole.
Rudi kwenye Sura
86. Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu aliye kuumba na akakulea, ni Mwenye
viumbe vyote, na anajua hali yako na yao. Yeye anastahiki umtegemezee mambo
yako na yao. Naye anajua maslaha yako na yao.
Rudi kwenye Sura
87. Ewe Nabii Muaminifu, tumekupa Aya saba za Qur'ani, nazo ni
Sura ya Al- Fatiha unayo ikariri katika kila Sala, na humo yamo ya kutunyenyekea
na maombi ya uwongofu yaliyo kaamili. Na tumekupa Qur'ani Tukufu yote.
Na ndani yake mna hoja, na miujiza. Kwa hivyo wewe una nguvu ambazo zinakufalia
usamehe.
Rudi kwenye Sura
88. Ewe Mtume! Usivitazame kwa kuvitamani na kuvitaka vitu vya starehe
ya dunia tulivyo wapa makafiri wa kishirikina, na Kiyahudi, na Kikristo,
na Kimajusi. Kwani hivyo ni duni kwa kulinganisha na ulio pewa wewe katika
kuwasiliana nasi, na Qur'ani Tukufu. Wala usiwasikitikie kwa sababu ya
kuendelea kwao na madhambi. Nawe tulia, na unyenyekee, na wachukue Waumini
ulio nao kwa upole. Kwani hao ni nguvu za Haki, na watu wa Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye Sura
89. Ewe Nabii! Waambie makafiri wote: Mimi nakuonyeni na adhabu kali,
na nakubainishieni maonyo yangu kwa hoja za kukata.
Rudi kwenye Sura
90. Haya ni kama maonyo ya walio igawanya Qur'ani wakaifanya ati
ni mashairi, na ukohani, na hadithi za kale na mengineyo. Nao wasiiamini
juu ya kusimama hoja juu yao.
Rudi kwenye Sura
91. Hao waliifanya Qur'ani vipande mbali mbali, nayo hali kuwa haikubali
kugawika kwa umuujiza wake na ukweli wake.
Rudi kwenye Sura
92. Ikiwa hiyo hali yao, basi Wallahi kwa Aliye kuumba akakulinda
na akakulea, hapana shaka tutawahisabu wote Siku ya Kiyama,
Rudi kwenye Sura
93. Kwa vitendo vyao vya kuudhi, na kufuru, na kejeli.
Rudi kwenye Sura
94. Basi wewe tangaza wito wa Haki, wala usishughulike na wayatendao
washirikina na maneno yao.
Rudi kwenye Sura
95. Na hao washirikina wanao ukejeli wito wako hawatokushinda, wala
hawatoweza kukuingilia kati baina yako na wito wako.
Rudi kwenye Sura
96. Hao washirikina mawazo yao yamedhoofika, ndio wakafanya kuwa
Mwenyezi Mungu anao miungu mingine ya masanamu. Na watakuja jua matokeo
ya ushirikina wao itapo wateremkia adhabu chungu.
Rudi kwenye Sura
97. Nasi tunajua dhiki ya moyo inayo kupata kwa wanayo yasema ya
ushirikina na kejeli na dharau.
Rudi kwenye Sura
98. Ikikupata dhiki hiyo mkimbilie Mwenyezi Mungu Mtukufu umwelekee,
na umt'ii na umnyenyekee, na utake msaada kwa Sala, kwani humo ndio imo
poza.
Rudi kwenye Sura
99. Na shikilia ibada ya Mwenyezi Mungu aliye kuumba, akakulinda,
mpaka ifike amri ya yakini, nayo ni Kiyama na miadi.
Rudi kwenye Sura