1. Enyi washirikina! Kuweni na yakini kwamba aliyo kuahidini
Mwenyezi Mungu kuwa yatakuwa Siku ya Kiyama yapo karibu kutokea bila
ya shaka. Basi msifanye maskhara kwa kuyahimiza yatokee. Mwenyezi Mungu
ametakasika na kuwa na mshirika wa kuabudiwa badala yake. Na hiyo miungu
mnayo mshirikisha naye haiwezi jambo lolote.
Rudi kwenye Sura
2. Mwenyezi Mungu huteremsha Malaika kwa yanayo huisha nyoyo katika
Wahyi wake (ndio hiyo Roho) juu ya anaye mkhiari kumpa Utume katika waja
wake, ili watu wajue kwamba hapana mungu wa kuabudiwa kwa Haki ila Mimi.
Basi jitengeni na yanayo nikasirisha na yatayo kuleteeni adhabu. Na shikamaneni
na ut'iifu ili ukukingeni na adhabu.
Rudi kwenye Sura
3. Yeye ameumba mbingu na ardhi kwa mujibu wa hikima. Ametakasika
kuwa na mshirika wa kufanya lolote katika utawala wake, au wa kuabudiwa
kama Yeye.
Rudi kwenye Sura
4. Amemuumba kila mmoja katika wanaadamu kutokana na maji maji yasiyo
shikamana, nayo ni manii. Kutokana na hayo ndio anakuwa mtu mwenye nguvu
za kujitetea nafsi yake, mshindani na makhasimu zake, mwenye kuweka wazi
hoja zake.
Rudi kwenye Sura
5. Enyi waja! Mwenyezi Mungu amekufadhilini - amekuumbieni nyama
hoa, wanyama wa kufuga, kama ngamia, na ng'ombe, na kondoo, na mbuzi,
ili mpate kutokana na sufi zao na manyoa yao vifaa vya kukupatieni joto
kujihifadhi na baridi, na mle nyama yao mhifadhi uhai wenu.
Rudi kwenye Sura
6. Na mnapata kwao raha na furaha mnapo waona wanarejea kutoka machungani
na matumbo yao na viwele vimejaa, na mnapo toka nao kwenda makondeni na
machungani wakikimbilia malisha yao.
Rudi kwenye Sura
7. Na wanakubebeeni mizigo yenu mizito mpaka kwenye miji ambayo hamwezi
kuifikilia bila yao isipo kuwa mzitie nafsi zenu katika juhudi na mashaka
makubwa. Hakika Mola wenu Mlezi aliye kutengenezeeni hayo yote kwa ajili
ya raha yenu bila ya shaka ni Mwingi wa upole, na Mkunjufu wa rehema kwenu.
Rudi kwenye Sura
8. Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni farasi, na nyumbu, na punda mpate
kuwapanda. Na mnawafanya ni pambo la kuingiza furaha katika nyoyo zenu.
Na Mwenyezi Mungu atakuja umba msivyo vijua sasa, katika vyombo vya kupanda
na vya kukata masafa miongoni mwa alivyo msahilishia Mwenyezi Mungu binaadamu
pindi akitumia akili yake na akafikiri kwayo, na akaongoka kwa kutumia
kila uwezo.
Rudi kwenye Sura
9. Na juu ya Mwenyezi Mungu, kwa mujibu wa fadhila yake na rehema
yake, kukuonesheni Njia Iliyo Nyooka ya kukufikisheni kwenye kheri. Na
zipo njia zilizo potoka zisio fika kwenye Haki. Na lau angeli taka kukuongoeni
nyote angeli kuongoeni kwenye Njia Iliyo Nyooka, lakini amekuumbieni akili
ya kutambua, na matakwa ya kuelekea, na akakuacheni na khiari yenu.
Rudi kwenye Sura
10. Yeye ndiye anaye teremsha maji kutoka jiha ya mbinguni. Katika
hayo mnapata kunywa, na mengine ndio inapelekea miti kumea. Nanyi hupeleka
wanyama wenu wakale kwenye miti hiyo, nao wakupeni maziwa, na nyama, na
sufi, na manyoa, na nywele.
Rudi kwenye Sura
11. Kwa maji yateremkayo mbinguni humea makulima ambayo tunakutoleeni
nafaka na mizaituni, na mitende, na mizabibu na mengineyo, katika kila
namna ya matunda mlayo mbali yaliyo tajwa. Hakika kuwepo vitu hivi ni alama
ya kuwaongoa watu wanao nufaika kwa akili zao, wakazingatia uwezo uliyo
patisha hayo.
Rudi kwenye Sura
12. Na Mwenyezi Mungu ameufanya usiku ukutumikieni kwa kuufanya uwe
ndio wakati wenu wa kupumzika na mchana ni muwafaka kuhangaika kwenu na
kwenda kwa kazi zenu, na jua kukuleteeni joto na mwangaza, na mwezi mpate
kujua idadi ya miaka na hisabu, na nyota zinazo kutumikieni kwa amri ya
Mwenyezi Mungu ili mpate kujua njia katika kiza. Hakika katika hayo zipo
alama na dalili kwa watu ambao wananufaika kwa akili aliyo wapa Mwenyezi
Mungu.
Rudi kwenye Sura
13. Na pamoja na aliyo kuumbieni Mwenyezi Mungu katika mbingu na
akakutengenezeeni kwa faida yenu, amekuumbieni pia juu ya ardhi wanyama
namna nyingi, na mimea, na vitu visio na uhai. Na ndani ya ardhi yamo maadeni
ya rangi na sura mbali mbali na faida mbali mbali. Na yote hayo kwa manufaa
yenu. Hakika katika hayo zipo dalili wazi na nyingi kwa watu wanao zingatia,
na wakawaidhika, na wakajua kwa hayo uwezo wa Aliye waumba, na rehema yake.
Rudi kwenye Sura
14. Ni Yeye aliye idhalilisha bahari, na akaifanya ikutumikieni,
mpate kuvua na mle nyama za samaki, laini na mpya mpya. Na mtoe humo baharini
mapambo kama lulu na marijani. Na ewe mwenye kuangalia ukazingatia, unaona
marikebu zinavyo pita baharini zikikata maji nazo zimesheheni bidhaa na
vyakula. Mwenyezi Mungu ameyadhalilisha hayo ili mnafuike nyinyi, na mtafute
riziki kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa njia ya biashara na nyenginezo,
na mpate kumshukuru kwa aliyo kutengenezeeni, na hayo ni kwa kukutumikieni
nyinyi.
Rudi kwenye Sura
15. Na Mwenyezi Mungu amefanya katika ardhi milima iliyo simama imara,
ili kuizuia isiyumbe yumbe.(Mwaka 1956 wataalamu wa geology, ilimu ya tabaka
za ardhi, wamegundua kuwa kweli milima inasaidia kuizuia ardhi isitaharaki
na kuachana. Wamevumbua kuwa mabara, continents, yamo katika kutaharaki.
Kwa mfano kusini ya Amerika iliambatana na Afrika ya Magharibi, na ilisota
mpaka ikafanyikana milima ya Andes. Hali kadhaalika Milima ya Himalaya
ikazuia kusota kwa Bara Hindi. Pia wamegundua kuwa maki ya gamba la ardhi
kwa kawaida halizidi kilomita 6, lakini chini ya milima hufika hata kilomita
35. Basi ni kweli kuwa milima ni kama vigingi vya kuzuia ardhi isiyumbe,
kama ilivyo sema Qur'ani miaka 1400 iliyo pita.)
Na Mwenyezi Mungu amefanya katika ardhi mito inayo pita na maji yanayo
faa kunywa na kunyweshea makulima, na njia zilizo tengenezwa ili mpate
kuzipitia kwendea mtakako.
Rudi kwenye Sura
16. Na Mwenyezi Mungu ameweka alama za kuwaongoza watu katika safari
zao kwenye ardhi, na hivyo wanapata uwongozi katika safari zao kwa nyota
ambazo ameziweka mbinguni ziwaongoze wanapo kuwa gizani hawazioni alama
za ardhini.
Rudi kwenye Sura
17. Hebu ni sawa kwa mwenye akili nzima baina ya Muweza na asiye
weza, hata akamfanya Mwenye kuumba yote haya sawa na asiye weza kuumba
kitu? Enyi washirikina! Hivyo hamzioni athari za uwezo wa Mwenyezi Mungu
mkazingatia na mkamshukuru kwazo Mwenyezi Mungu?
Rudi kwenye Sura
18. Na mkitaka kuzihisabu neema za Mwenyezi Mungu juu yenu, hamwezi
kuzidhibiti. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mkunjufu
wa rehema. Basi tubuni kwake, na mumsafie ibada, ili apate kukusameheni
na kukurehemuni.
Rudi kwenye Sura
19. Na Mwenyezi Mungu kwa ujuzi wake ulio kusanya kila kitu, anajua
mnayo yaficha na mnayo yadhihirisha. Na hapana chochote kinacho fichikana
kwake cha siri yenu na jahari yenu.
Rudi kwenye Sura
20. Huyu Muumba, na Mjuzi wa kila kitu, ndiye Yeye peke yake anaye
stahiki kuabudiwa. Ama hayo masanamu mnayo yaabudu, hayo hayawezi kuumba
chochote, hata nzi. Bali hayo yenyewe yameumbwa, na pengine mmeyaunda nyinyi
wenyewe kwa mikono yenu.
Rudi kwenye Sura
21. Na hayo ni vitu visivyo na roho kama maiti, hayana hisiya yoyote,
wala hayataharaki, wala hayajui Kiyama kitakuja lini, wala lini watafufuliwa
hao wanao yaabudu. Wala si laiki yenu, enyi wenye akili, baada ya haya
mkadhani kuwa yatakufaeni kitu hata mkayashirikisha na Mwenyezi Mungu katika
kuyaabudu.
Rudi kwenye Sura
22. Na imekwisha wekwa wazi kwa kila dalili kwamba hakika Mungu wenu
anaye pasa mumuabudu peke yake ni Mungu Mmoja ambaye hana mshirika wake.
Na juu ya hayo wale wasio amini kufufuliwa na kuhisabiwa, nyoyo zao zinaukataa
Upweke wake. Kiburi chao kinawazuia kufuata Haki na kuit'ii.
Rudi kwenye Sura
23. Hapana shaka kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayo yaficha na
wanayo yatangaza, ikiwa ni itikadi au maneno au vitendo. Naye atawahisabu
kwa yote hayo, na atawaadhibu kwa kiburi chao. Kwani hakika Yeye Subhanahu
hawapendi wanao jivuna hata hawataki kusikia Haki na kuifuata.
Rudi kwenye Sura
24. Na wakiulizwa hao makafiri wanao jivuna: Mola wenu Mlezi kamteremshia
nini Muhammad? Wao hujibu kwa inda: Hayo anayo dai kuwa Mwenyezi Mungu
kamteremshia si chochote ila uzushi na upuuzi walio tunga watu wa zamani
naye akayanukulu na akawa anayakariri tu.
Rudi kwenye Sura
25. Wanasema hayo ili wawazuie watu wasimfuate Mtume wa Mwenyezi
Mungu. Na mwisho wa kuishia mambo yao ni kuwa wataadhibiwa Siku ya Kiyama
kwa adhabu ya upotovu wao kwa ukamilifu, na adhabu ya baadhi ya watu walio
kuwa wakiwakhadaa na kuwadanganya mpaka wakapotea bila ya ilimu wala kuchungua!
Zingatia, ewe mwenye kusikia, kwa huu uovu wa madhambi wanayo yafanya,
vipi ukali wa adhabu watayo pata!
Rudi kwenye Sura
26. Na hawa makafiri wenye kiburi walitanguliwa na wengine mfano
wao. Walipanga njama zao kuwapangia Manabii wao, na wakafanya hila kuwapoteza
watu. Na Mwenyezi Mungu alizibomoa njama zao, akaiharibu miji yao. Akawateremshia
adhabu katika dunia ambayo hawakuitaraji.
Rudi kwenye Sura
27. Na kisha huko Akhera watapo fufuliwa watu na wakahisabiwa kwa
vitendo vyao, Mwenyezi Mungu atawasimamisha msimamo wa hizaya na fedheha,
atapo wafedhehi na afichue waliyo kuwa wakiyaficha vifuani mwao. Atawaambia:
Wako wapi hao miungu mliyo ifanya kuwa ni washirika wangu kwa kuwaabudu?
Nanyi kwa ajili yao mlikuwa mkinipiga vita Mimi na Mitume wangu!
Wako wapi wapate kukuungeni mkono, kama mlivyo kuwa mkidai? Hawatoweza
kujibu! Na hapo tena wale wanao ijua Haki, miongoni mwa Manabii, na Waumini,
na Malaika, watasema: Leo ndiyo hizaya na adhabu mbaya kabisa zitawashukia
makafiri!
Rudi kwenye Sura
28. Hizaya itawashukia makafiri walio endelea na ukafiri wao mpaka
Malaika walipo watoa roho, nao wamejidhulumu nafsi zao kwa ushirikina na
kutenda maovu, na wakasalimu amri tena baada ya inadi ndefu walipo jua
hakika ya makosa yao. Wakasema uwongo kwa jinsi walivyo shituka: Hatukuwa
duniani tukifanya maasi yoyote! Malaika na Manabii watawaambia: Hasha!
Hakika nyinyi ni waongo, bali mmetenda maasi maovu kabisa! Na Mwenyezi
Mungu, Subhanahu, anajua vyema kila dogo na kubwa mlilo kuwa mkilitenda
katika dunia yenu. Hakukuleteeni faida yoyote huko kukataa kwenu!
Rudi kwenye Sura
29. Na baada ya hayo wataambiwa: Mwisho wenu ni kuingia Motoni, na
adhabu ya huko ni ya milele, haikatiki! Na mbaya mno nyumba ya Jahannamu
kuwa ni makaazi ya kila mwenye kutakabari akakataa kufuata Haki na Imani
ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake.
Rudi kwenye Sura
30. Na walio muamini Mwenyezi Mungu na wakajikinga na kila linalo
mghadhibisha Yeye ikiwa neno, au kitendo, au itikadi, wataambiwa: Mola
wenu Mlezi kamteremshia nini Mtume wake? Wao watasema: Amemteremshia Qur'ani...ndani
yake mna kheri ya duniani na Akhera kwa watu wote, na kwa hivyo wakawa
miongoni mwa watu wema. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu huwalipa wema kwa maisha
mazuri katika uhai huu wa duniani. Na pahala pao Akhera ni bora na pazuri
zaidi kuliko waliyo yapata duniani. Na nyumba watayo ikaa wachamngu Akhera
ni hadi ya raha yake!
Rudi kwenye Sura
31. Nazo ni Bustani madhubuti za kudumu, zenye kupitiwa na mito chini
ya majumba na miti yake. Na hao watapata kila neema waipendayo. Na mfano
kama huu ndio malipo ya mema anayo walipa Mwenyezi Mungu wachamngu wote
wanao muamini, na wakajikinga na yanayo mkasirisha, na wakavifanya vyema
vitendo vyao.
Rudi kwenye Sura
32. Na ndio hao Malaika huzichukua roho zao na hali wamesafika na
uchafu wa ushirikina na maasi. Na Malaika watawaambia kwa kuwatuza: Amani
kwenu itokayo kwa Mwenyezi Mungu! Baada ya hii leo hamtopata la karaha.
Na ifurahieni Pepo mtakayo ingia kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo vitanguliza
katika dunia yenu.
Rudi kwenye Sura
33. Hao ndio wachamngu walio jitengenezea Akhera yao. Na hayo ndiyo
malipo yao. Ama washirikina kwa sababu ya inadi yao na kubakia kwao kwenye
ushirikina wao, hawataraji ila Malaika waje kunyakua roho zao nao wamezidhulumu
nafsi zao kwa ushirikina na vitendo vya shari. Na itawajia adhabu ya Mola
wako Mlezi iwateketeze wote. Na kama walivyo fanya makafiri hawa, basi
walikwisha wafanyia Manabii wao wale walio watangulia, na Mwenyezi Mungu
akawaadhibu kwa vitendo vyao. Wala Yeye hakuwadhulumu pale alipo waadhibu,
lakini wao wenyewe walizidhulumu nafsi zao walipo zitia katika adhabu kwa
ukafiri wao.
Rudi kwenye Sura
34. Yakawasibu malipo ya maovu waliyo yatenda, na adhabu waliyo kuwa
wakiikanya na kuikejeli ikawazunguka.
Rudi kwenye Sura
35. Na washirikina wakasema kwa inda na ukosefu: Lau kama Mwenyezi
Mungu angeli penda tumuabudu Yeye tu peke yake na tumt'ii kwa anayo tuamuru,
basi tusingeli muabudu mwenginewe, wala tusingeli harimisha sisi wenyewe
kitu asicho harimisha Yeye kama Bahira na Saiba. Na hii ni hoja potovu
wanayo itafutia njia katika ukafiri wao. Na makafiri walio kwisha tangulia
walitoa hoja kama hizo, baada ya kuwapelekea Mitume wetu, wakaamrisha Tawhidi
(kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja), na kumt'ii Yeye, na wakawakataza ushirikina
na kuharimisha asivyo harimisha Mwenyezi Mungu. Hoja ikasimama dhidi yao.
Na Mitume wetu wakatimiza tuliyo waamrisha wayafikishe. Na juu yetu kuwahisabu
wao. Na Mitume hawana jukumu zaidi ya hayo.
Rudi kwenye Sura
36. Na kila umma tuliwapelekea Mtume awaambie: Muabuduni Mwenyezi
Mungu peke yake. Na jitengeni na kila jabari mharibifu. Na wafikishie
ujumbe, na uwaongoze. Basi kikundi kikasikiliza uwongozi na kikafuata,
na Mwenyezi Mungu akakiongoa kwa kuwa kilijitayarisha vizuri kufuata Njia
Iliyo Nyooka. Na kikundi kingine kikapuuza kusikia Haki, kikastahiki kwenda
njia potovu, na Mwenyezi Mungu akakipelekea adhabu. Na ikiwa nyinyi, washirikina
wa Makka, mna shaka na haya, basi tembeeni katika nchi za karibu nanyi,
muangalie, mzingatie nini kilicho washukia wanao kanusha, kina A'ad na
Thamud na Kaumu Luut'i. Na vipi ilikuwa khasara yao na hilaki yao katika
mwisho wao!
Rudi kwenye Sura
37. Ewe Nabii! Ikiwa una hamu mno ya kuwaongoa washirikina katika
watu wako, kwa kutumia ukomo wa juhudi yako, basi usiihiliki nafsi yako
kwa huzuni ikiwa hayo uyatakayo hayawi. Kwani hao wamekwisha milikiwa na
matamanio. Na Mwenyezi Mungu hawalazimishi kuongoka walio khiari upotovu
na wakaushikilia, kwani Yeye huwaacha wajichagulie wenyewe, nao watapata
malipo yao, nayo ni adhabu kubwa. Na wala hawatapata Siku ya Kiyama wa
kuwanusuru na kuwalinda na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye Sura
38. Na washirikina juu ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu wameongezea
kuikanusha Siku ya Kiyama. Wameapa, ukomo wa nguvu zao za kuapa, na wakakazania
kwamba Mwenyezi Mungu hamfufui aliye kufa! Nao ni waongo katika viapo vyao,
na Mwenyezi Mungu atawafufua wote! Kwani Yeye amejichukulia ahadi mwenyewe,
na Mwenyezi Mungu kabisa hatokwenda kinyume na ahadi yake. Lakini watu
wengi miongoni mwa makafiri hawaijui hikima ya Mwenyezi Mungu katika kuumba
huu ulimwengu, na kwamba Yeye hakuumba kwa mchezo tu, wala wao hawajui
hisabu yake na malipo yake.
Rudi kwenye Sura
39. Hakika katika uadilifu wa Mwenyezi Mungu ni kuwa atawafufua wote
baada ya kufa kwao ili ipate wadhihirikia hakika ya mambo waliyo khitalifiana.
Waumini wapate kujua kuwa wao wako katika Haki, na makafiri wajue kwamba
wao walikuwa makosani kwa kumfanyia Mwenyezi Mungu washirika katika Ungu,
na pia ni waongo kwa kuapa kwao kwamba Mwenyezi Mungu hamfufui aliye kufa,
na ili yote makundi mawili yapate malipo yao kwa kujua na kwa sababu zake.
Rudi kwenye Sura
40. Na kuwafufua watu Siku ya Kiyama si jambo zito kwetu, hata hao
makafiri wakayaona hayawi. Kwani Sisi tutakapo kitu kiwe hatuna haja ya
lolote ila ni kusema tu: Kuwa! Na kinakuwa kama tutakavyo.
Rudi kwenye Sura
41. Na Waumini walio yaacha majumba yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu
Mtukufu, na usafi wa imani yao, baada ya kudhulumiwa na washirikina, tutawalipa
duniani, kwa ikhlasi yao na kustahamili kwao adhabu, maisha mema yasiyo
patikana ila kwa jihadi. Na Siku ya Kiyama ujira wao utakuwa mkubwa zaidi,
na neema zao za Peponi ni kubwa zaidi. Lau kuwa wapinzani wao wangeli jua
hayo wasingeli wadhulumu na wakazidhulumu nafsi zao.
Rudi kwenye Sura
42. Na hao Wahajiri (Walio hama) ndio walio vumilia adhabu walio
ipata kwa sababu ya Itikadi yao, na wakamwachia hali yao Mwenyezi Mungu
peke yake, bila ya kumbali mwenginewe. Kwa ajili ya hayo tumewapa
bora ya malipo.
Rudi kwenye Sura
43. Na kabla ya kukutuma wewe, ewe Nabii, kwa umma wako, hatukuwatuma
kwa kaumu zilizo tangulia ila watu wanaume tulio wafunulia kwa Wahyi yale
tunayo yataka wawafikishie. Wala hatukuwatuma Malaika kama watakavyo makafiri
wa kaumu yako. Basi, enyi makafiri, waulizeni wenye kuvijua Vitabu vya
mbinguni, kama nyinyi hamyajui hayo. Watajua kuwa Mitume wote wa Mwenyezi
Mungu hawakuwa ila wanaadamu, wala si Malaika.
Rudi kwenye Sura
44. Na hao Mitume tuliwaunga mkono kwa miujiza na dalili zilizo wazi
za kuthibitisha ukweli wao. Na tuliwateremshia Vitabu vya kuwabainishia
sharia zao zenye maslaha yao. Na wewe, ewe Nabii, tumekuteremshia Qur'ani
uwabainishie watu Itikadi na Hikima ziliomo ndani yake, na uwatake waizingatie,
kwa kutaraji kuwa watazingatia, na watawaidhika, na mambo yao yanyooke.
Rudi kwenye Sura
45. Yafaa vipi basi baada ya yote haya kuwa hao washirikina wakaendelea
katika inda yao, na wakampangia vitimbi Mtume? Je, kwani wamedanganyika
na upole wa Mwenyezi Mungu kwao, hata wakaitakidi kuwa wameaminika na adhabu
ya Mwenyezi Mungu, na ardhi haitowameza kama ilivyo mfanyia Qaaruun? Au
kuwa adhabu haitowajia kwa ghafla katika kimbunga kama ilivyo wapata kina
Thamud nao hawajui inatoka wapi?
Rudi kwenye Sura
46. Au ikawahiliki kati ya nyendo zao katika nchi kwa ajili ya biashara
nao wapo mbali na makwao, hata wasiweze kuikwepa adhabu ya Mwenyezi Mungu?
Kwani Yeye haemewi na chochote akitakacho!
Rudi kwenye Sura
47. Au akawateremshia adhabu katika nafsi zao na mali yao kidogo
kidogo, na hali wao kila wakati wa hiyo adhabu wamo katika khofu na kuingoja
iwateremkie. Basi, enyi washirikina! Msiendelee, mkajidanganya kwa kuchelewa
adhabu yenu! Upole wake Mwenyezi Mungu ulio enea, na rehema yake iliyo
kunjuka, ndio iliyo hukumu asikuleteeni kwa haraka adhabu ya hapa duniani,
ili mpate kufikiri na kuzingatia. Kwani Yeye Subhanahu ni Mpole na Mwenye
kurehemu.
*
Rudi kwenye Sura
48. Hao makafiri wameghafilika na Ishara za Mwenyezi Mungu zilizo
wazunguka. Wala hawatazami wakazingatia vitu alivyo viumba Mwenyezi Mungu
vilivyo tulia, na hali vivuli vyake vinakwenda. Mara vinanyookea kulia
na mara kushoto, vikifuata mwendo wa jua mchana, na mwendo wa mwezi usiku.
Na vyote hivyo vinat'ii amri ya Mwenyezi Mungu, vinafuata hikima ya mipango
yake. Na lau washirikina wangeli zingatia haya, wangeli jua kuwa Muumba
wake, na Mwenye kuyapanga ni Yeye peke yake anaye stahiki kuabudiwa na
kunyenyekewa, Muweza wa kuwahiliki akitaka.
Rudi kwenye Sura
49. Ni kwa Mwenyezi Mungu pekee - wala si kwa mwenginewe - hunyenyekea
na kut'ii vyote alivyo viumba mbinguni na viumbe viliomo na vyendavyo katika
ardhi. Na mbele yao ni Malaika wanao nyenyekea wala hawatakabari na kumt'ii.
Aya hii imeitangulia sayansi kwa kusema kuwa katika baadhi ya sayari
upo uhai katika mfumo huu wetu wa jua, au nje yake. Sayansi sasa inajaribu
kutaka kuvumbua hayo.
Rudi kwenye Sura
50. Na hali yao ni kuwa daima wamo katika kumkhofu Mola wao Mlezi,
Mwenye uwezo na nguvu, na wanafanya anayo waamrisha.
Rudi kwenye Sura
51. Mwenyezi Mungu amesema: Msiabudu wawili, wala msifanye miungu
wawili. Kwani kushiriki katika ibada kunapingana na Umoja wa kuumba.
Wa kuabudiwa kwa Haki ni Mungu Mmoja tu. Basi niogopeni Mimi wala msimkhofu
mwengine.
Rudi kwenye Sura
52. Yeye pekee ndiye mwenye vyote viliomo mbinguni na katika ardhi,
kwa kuviumba na kuvimiliki na kumuabudu. Basi ni haki yake Yeye tu pekee
kuabudiwa na kuhimidiwa na kunyenyekewa, na kutarajiwa rehema yake, na
kuogopwa adhabu yake.
Rudi kwenye Sura
53. Na neema yoyote ikikujieni, basi inatoka kwa Mwenyezi Mungu peke
yake. Kisha kikikupateni chochote cha kukudhuruni msiyayatike kwa ukomo
wa kelele zenu kwa mwenginewe yeyote isipo kuwa Yeye.
Rudi kwenye Sura
54. Kisha akiitikia maombi yenu na akakuondoleeni madhara baadhi
yenu huisahau Haki ya Mwenyezi Mungu ya Umoja wake na kumsafia ibada Yeye
tu, wakamshirikisha Muumba wao na Mlezi wao, na wakawaabudu naye wenginewe.
Rudi kwenye Sura
55. Hayo hutokea ili mwisho wao huwa kuikanya fadhila yetu kwa yale
tuliyo wapa. Basi enyi makafiri! Stareheni na hayo msiyo yatolea Haki ya
shukrani. Mtakuja kuujua mwisho wa ukafiri!
Rudi kwenye Sura
56. Na washirikina huyapa masanamu yao, ambayo wanayaita kwa ujinga
wao kuwa ni miungu, sehemu ya kujikaribisha kwayo kutokana na zile riziki
tulizo wapa Sisi, katika makulima na mifugo na vyenginevyo. Nakuulizeni,
kwa Utukufu wangu, enyi washirikina, hayo mliyo khitalifiana kwayo katika
uwongo wenu na upotovu mlio uzua. Na Mimi nitakulipeni kwayo.
Rudi kwenye Sura
57. Na hujaalia kumpa Mwenyezi Mungu yale wayachukiayo wao, kwa kudai
kuwa Malaika ni watoto wake wa kike, na wao wanawaabudu. Mwenyezi Mungu
apishe mbali na hayo! Na wao ati wanajipa wayapendayo nayo ni watoto wanaume.
Rudi kwenye Sura
58. Na akiambiwa mmoja wao kwamba amepata mtoto wa kike, uso wake
unasawijika kwa huzuni, naye amejaa hasira na amekasirika.
Rudi kwenye Sura
59. Anajaribu kujificha watu wasiione huzuni ya machungu yaliyo mpata
kwa kupewa khabari ya binti aliye zaliwa. Anatapatapa: amwache hai juu
ya fedheha anayo iona, kama anavyo jigamba? Au amzike katika udongo naye
yuhai mpaka afe? Ewe msikilizaji! Zingatia uwovu wa vitendo vya watu hawa!
Na uovu gani wa kumhukumia Mwenyezi Mungu mabinti ambao wao wanawachukia!
Rudi kwenye Sura
60. Ni hali mbaya ya wasio amini Akhera na yote yaliyoko huko ya
thawabu na adhabu, nayo ni ile haja ya kutaka watoto wa kiume na kuchukia
watoto wa kike. Na Mwenyezi Mungu ana sifa tukufu. Yeye ni Mkwasi, hahitajii
kitu, wala hana haja ya mtoto. Naye ni Mwenye kushinda, Mwenye nguvu, wala
hana haja ya msaidizi.
Rudi kwenye Sura
61. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli fanya haraka kuwaadhibu watu
kwa dhulma zao wanazo zifanya, basi asingeli mwacha hata mnyama mmoja juu
ya ardhi. Lakini Yeye kwa upole wake na hikima yake anawaakhirisha
madhaalimu mpaka wakati aliyo uweka, nao ndio wakati utapo kwisha muda
wao. Ukija wakati huo hawato taakhari hata kidogo, wala hawato tangulia.
Rudi kwenye Sura
62. Na washirikina wanamnasibisha Mwenyezi Mungu mabinti na ushirika
mambo ambayo wao wanayachukia. Na ndimi zao zinatamka uwongo wanapo dai
ya kwamba, kama walivyo kuwa na utajiri na utawala duniani, basi kadhaalika
Akhera nao watapata malipo mema kwa Mwenyezi Mungu watapo fufuliwa; nayo
ni Pepo! Hapana shaka hao watatiwa Motoni, nao watasukumwa huko kabla ya
wengineo.
Rudi kwenye Sura
63. Ewe Nabii! Jua kwa yakini kwamba Sisi tuliwatuma Mitume kabla
yako kwa kaumu nyingi kama tulivyo kutuma wewe kwa watu wote. Lakini Shetani
aliwapambia ukafiri, na ushirikina, na maasi. Basi wakawakanya Mitume wao,
na wakawaasi, na wakamsadiki Shetani na wakamt'ii yeye. Basi yeye amekuwa
ndiye mwenye kuyatawala mambo yao katika dunia, akiwapambia mambo ya kuwadhuru.
Na Akhera watapata adhabu yenye machungu makali.
Rudi kwenye Sura
64. Na hatukukuteremshia wewe hii Qur'ani isipo kuwa upate kuwabainishia
watu haki katika yale waliokhitalifiana kwayo katika dini, na ili ipate
kuwa ni uwongofu ulio timia na rehema ilio enea kwa kaumu yenye kumuamini
Mwenyezi Mungu na Kitabu alicho kiteremsha.
Rudi kwenye Sura
65. Na Mwenyezi Mungu ameteremsha kutoka mbinguni maji yanayo bebwa
na mawingu, akaifanya ardhi ikamea na ikawa na uhai, baada ya kuwa kabla
yake kavu haina uhai. Hakika katika hayo pana dalili wazi ya kuwepo Mwenye
kudabiri Mwenye hikima.
Maji huteremka kutoka mbinguni kuangukia ardhini, na huko
huyayusha chumvi chumvi zake za namna mbali mbali ambazo hunyonywa na mimea
kugeuka kwenye uhai.
Rudi kwenye Sura
66. Na enyi watu! Hakika katika nyama hoa, yaani mifugo, ngamia,
ng'ombe, na kondoo na mbuzi, mna mawaidha yanayo faa kuzingatiwa na kufuatwa
uwongofu wake wa kumtoa mtu ujingani akaingia kumjua Mwenye kuumba, Aliye
anzisha kila kitu, Mwenye hikima. Na Sisi tunakunywesheni kutokana na baadhi
ya viliomo matumboni mwa hao wanyama vilio zidi katika chakula na damu
maziwa safi, matamu, mepesi kuyapata kwa wanao kunywa.
Katika viwele vya wanyama wa mifugo imo namna ya mitoki (glands)
ambayo inachuja maziwa. Mitoki hiyo inanyweshwa na mishipa inayo leta madda
maalumu kutokana na damu, na (chyle); hicho ni chakula kilicho tayarishwa.
Viwili hivyo huwa vimekwisha lainishwa kwa kumezwa kama ni chakula. Kisha
hapo hizo glands za maziwa huteuwa sehemu yenye kuhitajiwa kwa kufanya
maziwa kutokana na vitu viwili hivyo, damu na chyle, na humiminiwa maji
maalumu kugeuza hivyo vikawa maziwa yenye kukhitalifiana na asili yake
kwa rangi na utamu kabisa.
Rudi kwenye Sura
67. Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu tuliyo kuneemesheni
kwayo na tukakuwezesheni kuitumia, mnakamua maji yake yakatoka ulevi usio
kuwa mzuri, na chakula kilicho kuwa kizuri. Hakika katika haya pana alama
yenye kuonyesha uwezo na rehema kwa watu wanao nafiika kwa akili zao. (Kitu
kile kile kina faida kikitumiwa kwa sharia za Mwenyezi Mungu za maumbile,
na kile kile kikawa na madhara kikitumiwa kinyume na hizo sharia.)
Rudi kwenye Sura
68. Ewe Nabii! Zingatia jinsi Mwenyezi Mungu alivyo mfahamisha nyuki,
kama kwamba amemfunulia kwa Wahyi, akamwonyesha sababu za uhai wake, na
njia za maisha yake. Akamfunza ajenge masega yake katika mapango, na katika
uwazi wa miti, na kwenye maburuji ya majumba na mizabibu.
Rudi kwenye Sura
69. Kisha Subhanahu akamhidi Nyuki ale matunda ya miti na mimea mbali
mbali, na akamsahilishia afuate njia alizo mtengezea Mola wake Mlezi, na
akatoa kutokana na matumbo yake kinywaji, nacho ni asali, chenye rangi
mbali mbali. Na hiyo asali imekuwa ni dawa ya kuwaponyesha watu. Hakika
katika hayo pana ufundi wa ajabu wa kuonyesha nguvu, na kuwepo Mwenye kuumba,
na Mwenye kuweza, Mwenye hikima. Wenye kutumia akili zao wananufaika kwa
mazingatio hayo, na watapata furaha ya daima.
Asali ya nyuki ni mchanganyiko wa glucose na livulose, nayo
ni namna ya sukari ambayo ni nyepesi kabisa kutumika mwilini, na madaktari
wamevumbua karibu kuwa glucose ina faida kutibu maradhi mengi, kwa kupiga
sindano, na kwa mdomo na kwa nyuma, kwa kuwa inatia nguvu, na inapinga
sumu ya maadeni kadhaa wa kadhaa, na sumu inayo patikana kwa maradhi ya
viungo, kama kuingia sumu kwa mkojo na maradhi ya kuwa manjano jaundice
na mengineyo. Vile vile imethibiti kuwa Vitamin nyingi hupatikana humo,
na khasa Vitamin B complex.
Rudi kwenye Sura
70. Mwenyezi Mungu amekuumbeni, na amekujaalieni kila mtu na ajali
yake. Kati yenu wapo wanao kufa mapema, na wengine wanao fikia ukongwe
wakarejea katika hali ya udhaifu. Wakawa wanadhoofika kidogo kidogo, zikipungua
nguvu zao za mwili, na mifupa na viungo na mishipa. Mwisho wao wakawa hawajiwezi
kujifanyia lolote liwapasalo! Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa siri
za kuumba kwake, ni Muweza wa kutimiza alitakalo.
Rudi kwenye Sura
71. Na Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu kwa riziki kuliko
wengineo. Amemruzuku bwana mwenye kumiliki kuliko mtumwa mamluki. Wala
walio ruzukiwa kingi hawawapi watumwa wao hata nusu ya riziki yao, ili
wapate kuwa wote na riziki sawa! Basi ikiwa hawa makafiri hawakubali watumwa
wao washirikiane nao katika riziki iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu, nao wote
ni wanaadamu kama wao, basi vipi wao wanataka kumshirikisha Mwenyezi Mungu
na viumbe vyake katika mambo yasio kuwa laiki naye Subhanahu wa Taa'la,
nako ni kustahiki kuabudiwa? Basi je, macho ya hao washirikina yataendelea
kufumbika baada ya yote haya, wakabaki wakipinga neema za Mwenyezi Mungu
juu yao kwa kumshirikisha Yeye na wengineo?
Rudi kwenye Sura
72. Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake wa jinsi yenu mtulie nao.
Tena amekupeni, kutoka kwa wake zenu, wana na wajukuu, na akakuruzukuni
vitu vya kufurahisha nafsi zenu alivyo kuhalalishieni. Je, baada ya haya
ndio baadhi ya watu humshirikisha Mwenyezi Mungu, na wakaamini upotovu,
na wakazipinga neema za Mwenyezi Mungu zinazo onekana, ambazo zinastahiki
shukrani kutoka kwao, na kumsafia ibada Mwenyezi Mungu?
Ndoa ni mfungamano mtakatifu ambao ndio asili ya ukoo na kiini cha
umma na jamii. Na ndoa ni mpango wa kuidhibiti ile khulka waliyo nayo wanaadamu
na wanyama, nayo ni kutamani kuingiliana. Lau ingeli kuwa hapana ndoa iliyo
kadiriwa kudhibiti ile khulka ya kutamaniana basi binaadamu wangeli kuwa
sawa na wanyama kwa kufuata fujo na uchafu wa kuingiliana. Na hapo mwanaadamu
asingeli kuwa yule kiumbe aliye mjaalia Mwenyezi Mungu kuwa na akili na
fikra na akamtukuza kuliko viumbe vyengine, na akamrithisha mamlaka ya
ardhi. Ilivyo kuwa mpango wa Mwenyezi Mungu katika uhai huu ni kutengeneza
khulka kwa ndoa ili binaadamu awe juu kuliko wanyama wengine, hali kadhaalika
binaadamu kwa upande mwengine ameumbiwa kupenda kubakia. Na ilivyo kuwa
hapana njia ya kubakia yeye mwenyewe, naye anayajua hayo kutokana na baba
zake na babu zake na vitu vyote vilio hai, basi njia pekee ni yeye kuzaa
dhuriya wapate kuishi na kuendelea daima.
Na labda lenye kuweka wazi kabisa ile khulka yake ni kauli ya Mwenyezi
Mungu Mtukufu: "Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu,
na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akakuruzukuni
vitu vizri vizuri."
Rudi kwenye Sura
73. Na wakawa badala ya Mwenyezi Mungu wakaabudu masanamu ambayo
hayawezi kuwapa riziki yoyote hata chembe, sawa sawa ikiwa riziki hiyo
inatoka mbinguni kama maji, au kutokana na ardhi kama matunda ya miti na
mimea. Na miungu hiyo haiwezi kufanya lolote kama hayo, wala duni ya hayo!
Rudi kwenye Sura
74. Na ilivyo kuthibitikieni kuwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu hakufaeni
kitu, basi msiseme kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ana yeyote wa kumshabihi,
ikawa kisingizio cha kuwaabudu hao kwa vipimo vipotovu, na kushabihisha
kusio kweli kwa ajili ya kuwaabudu hao pamoja naye! Hakika Mwenyezi Mungu
anajua upotovu wa mnayo yatenda, naye atakulipeni kwayo na hali nyinyi
mmo katika mghafala hamjui ubaya wa mwisho wenu!
Rudi kwenye Sura
75. Mwenyezi Mungu amepiga mfano kufahamisha ufisadi walio nao
washirikina. Mtumwa aliye milikiwa kama mtumwa mamluki, hanalo aliwezalo
kulitenda; na muungwana anaye ruzukiwa na Mwenyezi Mungu riziki ya
halali, naye anatoa katika hiyo riziki kwa siri na dhaahiri! Je, ni sawa
watumwa wasio weza kitu, na waungwana wenye nacho na wanatumia walicho
nacho? Hakika Mwenyezi Mungu anamiliki kila kitu, na anafanya katika ufalme
wake kama apendavyo. Na asiye kuwa Yeye hamiliki chochote. Basi huyo hastahiki
kuabudiwa na kuhimidiwa. Sifa zote ni haki ya Mwenyezi Mungu peke yake.
Yeye ndiye Mwenye Utukufu peke yake, kwani kila kheri inatoka kwake, na
kila zuri linarejea kwake. Wala hawatendi hao wanayo yatenda kwa kujua,
bali wanatenda kwa kuwafuata wakubwa zao. Bali wengi wao hawajui, na wanaziambatisha
neema za Mwenyezi Mungu kwa wengineo, na wanawaabudu hao badala yake!
Rudi kwenye Sura
76. Mwenyezi Mungu amekupigieni mfano mwengine, wa watu wawili. Mmoja
wao kiziwi-bubu; hafahamu wala hafahamiki, mzigo kwa aliye mlazimu kumtazama.
Bwana wake akimuelekeza kokote harejei na faida yoyote. Basi, je, mtu huyu
atakuwa sawa na mtu mwenginewe aliye fasihi wa kusema, anasikia vyema,
anaamrisha haki na uadilifu, naye mwenyewe ameshika Njia iliyo kaa sawa,
isiyo kwenda upogo? Huyo kiziwi asiye sikia wala kusema wala hafahamu wala
hafahamiki, ndio mfano wa masanamu wanayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu.
Kwani hayo hayasikii wala hayasemi wala hayafai kitu. Hayawezi hayo kulingana
na Mwenye kusikia, Mwenye kujua, Mwenye kuwaita watu wende kwenye kheri
na haki, na kwenye Njia Iliyo Nyooka.
Rudi kwenye Sura
77. Na ni ya Mwenyezi Mungu tu peke yake yote wasiyo yajua waja katika
mbingu na katika ardhi. Wala jambo la kuja Siku ya Kiyama, na kufufuliwa
watu, haraka yake na upesi wake kwa Mwenyezi Mungu, si chochote ila
ni kama kufumba na kufumbua jicho! Bali ni duni kuliko hivyo, jinsi ya
upesi wake. Hakika uwezo wa Mwenyezi Mungu ni mkubwa mno, Yeye haemewi
na kitu.
Rudi kwenye Sura
78. Na Mwenyezi Mungu amekutoeni kutokana na matumbo ya mama zenu
hali hamjui chochote katika yaliyo kuzungukeni. Na akakupeni kusikia
na kuona na nyoyo, kuwa ndio silaha za kujifunzia na kufahamu, ili mpate
kumuamini kwa njia ya ilimu, na mumshukuru kwa alivyo kufadhilini.
Utabibu wa kisasa umethibitisha kuwa kuweza kusikia kunaanza
mapema sana katika maisha ya mtoto mchanga, mnamo wiki chache za mwanzo.
Ama kuona huanza mwezi wa tatu. Wala kuona hakuwi baraabara mpaka katika
mwezi wa sita. Ama "moyo " wa kufahamu na kutambua huwa baada ya hayo.
Mpango ulio letwa na Qur'ani ni mpango unao lingana na hisiya hizo.
Rudi kwenye Sura
79. Je! Hao washirikina hawawaangalii ndege walio jaaliwa waweze
kuruka hewani juu, kwa kupewa na Mwenyezi Mungu mbawa kubwa kuliko miili
yao, wakiikunjua na kuikunja. Na Mwenyezi Mungu akaidhalilisha hewa kuwabeba
hao ndege. Hapana anaye washika huko angani ila Mwenyezi Mungu kwa nidhamu
aliyo itengeneza Yeye Mwenyewe! Hakika katika kuwatazama hao ndege, na
kuzingatia hikima ya Mwenyezi Mungu katika kuwaumba, ni ishara kubwa ya
kuwanafiisha walio kuwa tayari kuamini.
Ndege wanaruka kwa sababu kadhaa wa kadhaa katika kuumbwa
kwao. Muhimu kuliko yote ni lile umbo lao la kuchongoka, na kuwa mbawa
zao zilivyo tanda zenye manyoya, na mafupa yenye uwazi na myepesi na vifuko
vya hewa kati ya matumbo yao, navyo vimeambatishwa na mayavuyavu (mapafu).
Hivyo vifuko hujaa hewa wakati wa kuruka, basi huzidi hao ndege kuwa wepesi.
*
Rudi kwenye Sura
80. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ndiye aliye kujaalieni
mkaweza kusimamisha nyumba zenu ili ziwe maskani yenu. Na akakujaalieni
kutokana na ngozi za ngamia, na ng'ombe, na kondoo na wanyama wengineo
mkafanya mahema ambayo ni kama nyumba za kukalia, na mkihama nayo mnapo
safiri na mnapo tua. Na kutokana na sufi zao, na nywele zao, na manyoya
yao, mkafanya matandiko ya kutumia hapa duniani mpaka itakapo fika ajali
yenu ya kuondoka.
Rudi kwenye Sura
81. Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni miti na vitu vyenginevyo vya kukupeni
vivuli kukulindeni na taabu ya joto, na amekufanyieni mapango milimani,
nanyi mkafanya humo maskani kama nyumba. Pia amekuumbieni nguo za sufi
na pamba na kitani na vyenginevyo, ili kukuhifadhini na joto la jua, na
nguo za chuma za kukulindeni katika vita na adui zenu. Kama alivyo kujaalieni
hayo, basi kadhaalika amekutimizieni neema zake kwa kukupeni Dini iliyo
simama sawa, ili mpate kuifuata amri yake, na mumsafie ibada Yeye tu si
na mwenginewe.
Rudi kwenye Sura
82. Wakikupuuza, ewe Nabii, hao unao waita wafuate Uislamu, basi
wewe huna jukumu kwa mapuuza yao. Haikulazimu wewe ila kufikisha ujumbe
kwa uwazi, na hayo umekwisha fanya.
Rudi kwenye Sura
83. Kupuuza kwao hao makafiri si kwa kuwa hawajui kwamba Mwenyezi
Mungu Subhanahu ndiye chanzo cha kila neema zote wanazo zipata, lakini
wao hutenda vitendo vya wanao kanya neema, kwa vile hawamshukuru Mola Mlezi
kwazo. Na wengi wao wamekazania kuwafuata baba zao katika kumkataa Mwenyezi
Mungu, mpaka wakawa wengi wao ndio wapinzani.
Rudi kwenye Sura
84. Ewe Nabii! Mhadharishe kila anaye mkataa Mola wake Mlezi kwa
yatakayo tokea Siku tutakapo muinua kutokana na kila umma shahidi wa kuwashuhudia
kwa walivyo mpokea Mtume wa Mola wao Mlezi. Na pindi akitaka kafiri kutoa
udhuru, hatapewa ruhusa ya kutaka kutoa udhuru. Wala hatapatikana mwombezi
wa kumtengenezea maombezi, kwa kutakiwa warejee waache sababu za Mwenyezi
Mungu kuwakasirikia. Kwani Akhera sio pahala pa kutubia.
Rudi kwenye Sura
85. Na wale walio jidhullumu nafsi zao kwa kukufuru watakapo iona
Jahannamu, na wakataka wapunguziwe adhabu, hawato jibiwa, wala hawato akhirishwa
kuingia Jahannamu hata dakika moja.
Rudi kwenye Sura
86. Na walio wafanya miungu yao washirika wa Mwenyezi Mungu na wakawaabudu
watapo sema: Ewe Mola Mlezi wetu! Hawa ndio washirikishwa wetu tulio tukiwaabudu
kwa makosa. Basi tupunguzie adhabu kwa kuwapa wao baadhi ya adhabu!
Washirikishwa wao watajibu: Ama hakika nyinyi washirikina waongo kwa kudai
kwenu kuwa sisi ni washirika wa Mwenyezi Mungu, na kwamba nyinyi mkituabudu!
La kweli ni kuwa mkiabudu matamanio yenu tu, wala sisi hatukuwa washirika
kama mlivyo dai. (Nabii Isa a.s. amesema: "Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua
ninyi kamwe, ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu." - Injili ya Mathayo
7.21-27)
Rudi kwenye Sura
87. Hapo tena wale washirikina walio mshirikisha Mwenyezi Mungu watasalimu
amri, waikubali hukumu yake, na yawaondokee yale mawazo yao kwamba walio
kuwa wakiwaabudu yatakuja waombea na kuwakinga na adhabu!
Rudi kwenye Sura
88. Walio kufuru na wakawazuia wengine kufuata Njia ya Mwenyezi Mungu,
nayo ndiyo Njia ya kheri na haki, tutawazidishia adhabu juu ya adhabu wanayo
stahiki kwa ukafiri wao, kwa walivyo kusudia kuwafisidi na kuwapotosha
waja wa Mwenyezi Mungu!
Rudi kwenye Sura
89. Ewe Nabii! Wahadharishe makafiri katika kaumu yako kwa yatakayo
wapata Siku tutapo watolea kila umma shahidi wa kuwashuhudia, naye ndiye
Nabii wao, ambaye atakuwa ni mmoja wao, ili wawe hawana kisingizio. Na
wewe, ewe Nabii, tutakuleta uwashuhudie hao walio kukadhibisha. Na tangu
hivi sasa yawapasa wazingatie! Sisi tumekuteremshia wewe Qur'ani, ambayo
ndani yake kila kitu kimebainishwa kwa haki. Na ndani yake umo uwongofu,
na rehema, na bishara ya Pepo kwa wenye kuifuata na kuiamini.
Rudi kwenye Sura
90. Mwenyezi Mungu anawaamrisha waja wake uadilifu wa maneno na vitendo,
na katika kila jambo wakusudie lilio bora, na walifadhilishe kuliko jenginelo.
Kama anavyo amrisha kuwapa jamaa zenu wanacho hitajia, ili kuzidi kutia
nguvu makhusiano ya mapenzi kati ya ukoo. Na Mwenyezi Mungu anakataza kutenda
kila la makosa, na khasa madhambi yaliyo pita mpaka kwa ubaya, na kila
kisicho pendeza katika sharia na akili nzuri. Hali kadhaalika anakataza
kumfanyia uadui mtu. Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika anakukumbusheni haya,
na anakuelekezeni kwenye mambo mema, mpate kukumbuka fadhila zake kwa maelekezo
yake mema,basi ndio mfanye anavyo kwambieni.
Rudi kwenye Sura
91. Na timizeni ahadi mlizo jitolea nafsi zenu kwa kumshuhudisha
Mwenyezi kuwa mtazitekeleza, maadamu ahadi hizo ni kwa mujibu wa sharia
ya Mwenyezi Mungu. Wala msivunje viapo vyenu kwa kutotimiza baada ya kuvitilia
nguvu kwa kumtaja Mwenyezi Mungu, na kuazimia kikweli kutimiza. Nanyi mlipo
toa ahadi mlitia maanani kuwa Mwenyezi Mungu ndiye dhamini wenu kwamba
mtatekeleza, na kwamba Mwenyezi Mungu anakuangalieni na kukuoneni. Basi
shikamaneni na ahadi zenu na viapo vyenu, kwani Mwenyezi Mungu Subhanahu
anakujueni yupi katika nyinyi anaye timiza na anaye kwenda kinyume, yupi
anaye tekeleza na yupi anaye vunja. Basi atakulipeni kwa mnayo yafanya.
Rudi kwenye Sura
92. Wala msiwe katika kwenda kinyume na viapo vyenu baada ya kuvithibitisha
mfano wa mwanamke mwendawazimu anaye sokoto sufi, ikisha kuwa nyuzi akazifumua
tena. Mkafanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganya na kukhadaa watu,
na huku mkijitafutia udhuru kwa kuwa ama nyinyi ni wengi zaidi au mna nguvu
zaidi kuliko wao, au mnakusudia kuwaunga mkono maadui wenye nguvu zaidi
kuliko wao, au kwa kuwa mnataraji kuzidi nguvu kwa khiana! Na hakika Mwenyezi
Mungu anakufanyieni mtihani. Mkikhiari kutimiza ahadi mtapata mavuno ya
duniani na Akhera. Mkielekea khiana, basi ni khasara yenu. Na hakika Siku
ya Kiyama atakubainishieni ukweli wa khitilafu zenu za duniani, na atakulipeni
kwa mujibu wa vitendo vyenu.
Aya mbili hizi zinaonyesha kuwa msingi wa makhusiano baina
ya Waislamu na wengineo pamoja na uadilifu ni kutimiza ahadi, na kwamba
makhusiano baina ya mataifa hayasimami sawa ila kwa kutimiza ahadi, na
kwamba dola za Kiislamu zikijifunga kwa mapatano basi zijifunge kwa jina
la Mwenyezi Mungu. Maana ya hayo ni kuwa inakuwapo yamini ya Mwenyezi Mungu
na kuwa Yeye ndiye dhamini. Na Aya inafahamisha mambo matatu, ambayo lau
kuwa mataifa yangeli yatimiza basi amani ingeli enea:
* Kwanza: Haifai mapatano kuwa ndio njia ya kufanya khadaa. Ikiwa
hivyo inakuwa ni udanganyifu. Na udanganyifu haufai katika makhusiano baina
ya wanaadamu, sawa sawa ikiwa baina ya mtu na mtu, au kikundi na kikundi,
au baina ya madola.
* Pili: Kutimiza ahadi peke yake ni nguvu. Na mwenye kuvunja ahadi
ni kama mwenye kuvunja alicho kijenga kwa sababu za nguvu. Basi anakuwa
kama mpumbavu anaye tatua uzi wake kila akisha usokota.
* Tatu: Haimfalii mtu kuvunja ahadi kwa sababu ya kutafuta nguvu
au kutaka kuzidisha kipande cha ardhi.
Rudi kwenye Sura
93. Mwenyezi Mungu ange taka angeli kufanyeni nyote umma wa namna
moja kwa jinsi, na rangi, na imani, bila ya khitilafu. Na hayo ni kwa kukupeni
umbo jengine, mkawa kama Malaika wasio na uwezo wa kukhiari watakalo. Lakini
ametaka muwe jinsi na rangi mbali mbali, na akakupeni uwezo wa kukhiari
wenyewe. Mwenye kukhiari matamanio ya dunia kuliko kumridhi Mwenyezi Mungu,
anaachwa kwa ayatakayo. Na mwenye kutaka kumridhi Mwenyezi Mungu kwa vitendo
vyema, anasahilishiwa kwa anayo yataka. Na kuweni na yakini kuwa nyote
nyinyi mtakuja ulizwa Siku ya Kiyama juu ya mliyo yatenda duniani, na mtalipwa
kwa vitendo vyenu.
Rudi kwenye Sura
94. Wala msishike njia ya khiana, mkafanya viapo ndio njia ya udanganyifu
na khadaa. Kwa hivyo nyayo zenu zitateleza mlikosee lengo lilio sawa, na
kwa hivyo ikapelekea mkaiwacha Njia ya Mwenyezi Mungu ya kutimiza ahadi,
na mkawa ni mfano muovu wa khiana, na watu wakaja waona kuwa Waislamu ni
watu wabaya, na wakautupilia mbali Uislamu wenyewe. Na uovu ukateremka
duniani kwa sababu yenu kwa kuto kuaminini kwa vile mnavyo kwenda kinyume
na njia ya haki, nanyi ikakuteremkieni adhabu kali yenye kutia machungu.
Rudi kwenye Sura
95. Wala msibadilishe ahadi ya kweli kweli kwa kutaka pato la dunia,
na hilo ni duni na lingali onekana kubwa. Maana yaliopo kwa Mwenyezi Mungu,
malipo ya wanao hifadhi ahadi zao duniani, na malipo ya Akhera ya milele,
ni bora kwenu kuliko yote yanayo kudanganyeni kwa kuvunja ahadi. Basi zingatieni
na mfahamu, ikiwa nyinyi ni watu wa ilimu na utambuzi baina ya jema na
lisio kuwa jema. Wala msitende ila lilio na maslaha kwenu duniani na Akhera.
Rudi kwenye Sura
96. Kwani neema mlizo nazo zina mwisho hata zingeli kaa muda mrefu.
Na neema zilioko kwa Mwenyezi Mungu Akhera ni za milele wala hazishi. Na
Sisi tutawalipa wenye kuvumilia mashaka ya taabu kwa ajili ya tuliyo waahidi,
nayo ni kupata bora ya malipo marudufu kwa vitendo vyao, waneemeke kwayo
daima milele Akhera.
Rudi kwenye Sura
97. Hakika mwenye kutenda mema duniani, sawa sawa akiwa mwanamume
au mwanamke, akajiingiza katika huo wema kwa nguvu za imani, kwa kila linalo
wajibika kwa kuliamini, basi Sisi hatuna budi kumfanya aishi maisha mazuri
yasiyo kuwa na machungu, yenye ndani yake ukinaifu na kuridhika na kuvumilia
masaibu ya dunia, na shukrani kwa neema anazo zipata kwa Mwenyezi Mungu.
Na Akhera hapana budi ya kuwa tutawalipa watu wa namna hii bora ya malipo
kwa kuzidi marudufu kwa vitendo vyao vya duniani.
Rudi kwenye Sura
98. Kinacho linda nafsi isighurike na pumbao ni Qur'ani. Ewe Muumini!
Ukitaka kuishi maisha ya mbali na kuchezewa na Shetani, na upate
wema wa kote kuwili, duniani na Akhera, basi Mimi nakuongoza kwenye jambo
litakalo kusaidia kwa hayo. Jambo lenyewe ni kuisoma Qur'ani. Na
unapo taka kusoma Qur'ani, anzia kwa kumuomba Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi
akuepushe na wasiwasi wa Shetani, aliye fukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi
Mungu, na anaona uzuri kuwaghuri watu awaingize katika kumuasi Mwenyezi
Mungu.
Rudi kwenye Sura
99. Ukifanya haya kwa kumsafia niya Mwenyezi Mungu, basi atakulinda
na Shetani, na atakuondolea wasiwasi. Kwani Shetani hana athari kwa walio
jaa Imani ya Mwenyezi Mungu, na wakamtaka msaada na kumtegemea Yeye peke
yake.
Rudi kwenye Sura
100. Bali taathira yake Shetani na khatari yake ni juu ya wale ambao
nyoyo zao hazina mfungamano wala mapenzi na Mwenyezi Mungu. Basi hao hawana
la kuwalinda na athari za Shetani. Watamfuata huyo kama rafiki anavyo mfuata
rafiki yake, mpaka watumbukie katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika
kumuabudu pamoja na miungu mingine isiyo weza kuleta madhara wala manufaa.
Rudi kwenye Sura
101. Na tukikuletea muujiza badala ya muujiza ulio sawa na tulio
waletea Manabii walio tangulia, na tukakuletea wewe hii Qur'ani kuwa ni
muujiza wenyewe, wanakusingizia kuwa umeizua tu hii, na kwamba unamzulia
Mwenyezi Mungu uwongo! Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mjuzi kwa ujuzi
usio pikuliwa kuijua miujiza anayo wateremshia Manabii wake. Lakini wengi
wao watu hawa si watu wa ilimu wa kujua lilio kweli.
Rudi kwenye Sura
102. Ewe Nabii! Waambie kuwabainishia muujiza wako: Hakika hii Qur'ani
kaniteremshia mimi Jibril, Roho safi, kutokana kwa Mola wangu Mlezi, kwa
kufuatana na kukusanya Haki, ili kwayo azitie imara nyoyo za Waumini, na
ili iwe ni Uwongofu kwa watu wote waongokewe, na iwape bishara njema ya
neema Waislamu wote.
Rudi kwenye Sura
103. Hakika Sisi tunajua wayasemayo makafiri wa Makka, nayo: Hamfundishi
Muhammad hii Qur'ani ila mtu tunaye mjua, naye ni kijana wa Kirumi. Wala
hamteremshii Malaika kutoka kwa Mwenyezi Mungu kama asemavyo! Na kauli
yao hii ni ya uwongo. Kwani huyo kijana wanaye sema kuwa anakufundisha
wewe ni mgeni, hajui Kiarabu vizuri. Na Qur'ani ni lugha ya Kiarabu kilicho
wazi cha ufasihi, hata imekuwa nyinyi wabishi mmeshindwa kuleta mfano wake.
Basi hizo tuhuma zenu zina maana gani?
Rudi kwenye Sura
104. Hakika hao wasio zikubali Ishara za Mwenyezi Mungu ambazo wameshindwa
kuleta mfano wake, na wakashikilia kuzikataa juu ya kuemewa kwao, Mwenyezi
Mungu hawaongoi. Nao Akhera watapata adhabu kali kwa sababu ya ukafiri
wao na inadi yao!
Rudi kwenye Sura
105. Hakika wanao jasirisha kumzulia Mwenyezi Mungu uwongo ni wale
wasio ziamini Ishara za Mwenyezi Mungu, na hao peke yao ndio walio fikilia
ukomo wa uwongo. Na wewe, Nabii, si katika watu hao hata wa kutuhumie hivyo.
Rudi kwenye Sura
106. Hao wanao tamka ukafiri baada ya kuamini watapata ghadhabu ya
Mwenyezi Mungu. Isipo kuwa aliye lazimishwa kutamka maneno ya ukafiri na
hali moyo wake umesimama imara katika Imani. Huyo atavuka, haitompata ghadhabu
ya Mwenyezi Mungu. Ama ambao nyoyo zao zinafurahia ukafiri, na ndimi zao
zinakubaliana na yaliyo nyoyoni mwao, hao watapata ghadhabu kali
kwa Mwenyezi Mungu ambaye amewaandalia adhabu kubwa katika Akhera.
Rudi kwenye Sura
107. Na hiyo ghadhabu na adhabu waliyo stahiki kuipata, ni kwa sababu
ya kupenda kwao mno neema za duniani na starehe zake za kupita njia, hata
zikawaweka mbali na Haki, na zikawatia upofu wasiione kheri. Basi Mwenyezi
Mungu akawaachilia mbali na huo ukafiri wanao upenda. Huo ndio mwendo wake
anavyo watendea viumbe vyake, huwaacha kama hawa, na huwaacha asiwahidi
kwa sababu ya ufisadi wao wenyewe, na kukakamia katika upotovu.
Rudi kwenye Sura
108. Hao ndio Mwenyezi Mungu amewapiga muhuri wa mghafala katika
nyoyo zao, hata zikawa haziikubali Haki, na katika masikio yao wakawa hawasikii
kwa sikio la fahamu na mazingatio wakawa kama viziwi, na katika macho yao
hata wakawa hawaoni ishara na dalili zilio mbele yao. Hao ndio walio zama
katika kughafilika na Haki. Hao hawana kheri mpaka uondoke mghafala katika
akili zao.
Rudi kwenye Sura
109. Hao hapana shaka yoyote ndio peke yao watakao khasiri kila kheri
katika Akhera!
Rudi kwenye Sura
110. Tena, ewe Nabii! Jua kuwa Mola wako Mlezi ni Mwenye kuwasaidia
na kuwanusuru walio hama Makka kukimbiza Dini yao isikandamizwe, na nafsi
zao zisiadhibiwe na washirikina. Kisha wakapigana Jihadi kwa kadiri ya
uwezo wao, kwa maneno na vitendo, wakavumilia mashaka na taabu, na yaliyo
wakuta kwa ajili ya Dini yao. Hakika Mola wako Mlezi baada ya hayo waliyo
yastahamilia ni Mwenye kuwasamehe wakitubu, Mwenye kuwarehemu, basi hato
wachukulia kwa walio lazimishwa kuyafanya.
Rudi kwenye Sura
111. Ewe Nabii! Watajie watu wako, kwa kuwahadharisha, Siku ambayo
kila mtu atakuwa hana linalo mshughulisha ila kujitetea nafsi yake. Hayamshughulishi
ya mzazi wala mwana. Siku hiyo ndiyo Siku ya Kiyama! Na Mwenyezi Mungu
siku hiyo atailipa kila nafsi malipo ya vitendo iliyo tenda, ikiwa kheri
au shari. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu hata mtu mmoja.
Rudi kwenye Sura
112. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu amewapigia mfano watu wa Makka kisa
cha mji mmojapo. Watu wake walikuwa wamekaa kwa amani, hawana adui anaye
waingilia. Wametua, hawana dhiki ya maisha, riziki inawajia kwa wasaa kutoka
kila pahali. Wakazibeua neema za Mwenyezi Mungu, wasimshukuru kwa kumt'ii
na kutekeleza amri zake. Mwenyezi Mungu akawapatiliza kwa masaibu yaliyo
wazunguka kila upande. Wakaonja uchungu wa njaa na vitisho, baada ya utajiri
na amani walio kuwa nayo. Na hayo kwa sababu ya kukakamia kwao katika ukafiri
na maasi.
Rudi kwenye Sura
113. Nao alikwisha wajia Mtume kutokana nao wenyewe. Ilikuwa ni waajibu
wao wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hayo, lakini walimwambia mwongo, kwa
inda na husda tu. Adhabu ikawatwaa nao hali wamo katika udhalimu, na kwa
sababu ya hiyo dhulma.
Rudi kwenye Sura
114. Ikiwa washirikina wanazikufuru neema za Mwenyezi Mungu na wanazigeuza
kuwa ni nakama, basi nyinyi Waumini elekeeni kwenye shukra. Na kuleni katika
alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu na akakufanyieni kuwa ni vizuri kwenu,
wala msijiharimishie nafsi zenu. Na ishukuruni neema ya Mwenyezi Mungu
iliyo juu yenu kwa kumt'ii Yeye tu peke yake, ikiwa kweli mnamkusudia Yeye
tu kwa ibada.
Rudi kwenye Sura
115. Kwani hakika Mwenyezi Mungu hakukuharimishieni isipo kuwa nyamafu,
na damu inayo tiririka kutokana na mnyama wakati wa kumchinja, na nyama
ya nguruwe, na kilicho chinjwa kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini mwenye
kulazimishwa na shida ya njaa kula kitu alicho kuharimishieni Mwenyezi
Mungu, bila ya kutaka, na wala bila ya kupita hadi ya kiasi cha kuondoa
ile dharura, basi hakika Mwenyezi Mungu hayachukulii hayo. Kwani Yeye Subhanahu
ni Mwenye kuwasamehe waja wake. Huwasamehe wanapo tumbukia katika makosa
wasio endelea nayo. Naye ni Mwenye kuwarehemu kwa vile anawazuia vitu vinavyo
wadhuru, na anawaruhusu kwa kuhifadhi uhai wao.
Rudi kwenye Sura
116. Na ilivyo kuwa Mwenyezi Mungu amekwisha kubainishieni kilicho
halali na kilicho haramu, basi shikamaneni na hayo aliyo kubainishieni,
wala msithubutu kuhalalisha na kuharimisha ovyo kufuata ndimi zenu. Mkawa
mnasema: Hichi halali, na hichi haramu. Matokeo ya hizo kauli zenu ni kumzulia
uwongo Mwenyezi Mungu, na kumkhusisha na asiyo yasema! Hakika wanao mzulia
uwongo Mwenyezi Mungu hawapati kheri wala mafanikio.
Rudi kwenye Sura
117. Wakiendelea kufuata matamanio yao ya kidunia, basi hakika starehe
yao hiyo ni chache na haina dawamu, na Akhera watapata adhabu kali.
Rudi kwenye Sura
118. Wala hawakuharimishiwa ila Mayahudi tu vile vitu tulivyo kusimulia,
ewe Nabii, kabla ya kuteremka Aya hizi. Na vitu hivyo ni kuwa kila mnyama
mwenye makucha, na shahamu za ng'ombe na kondoo, ila ilio beba migongo
yao au matumbo, au iliyo changanyika na mifupa. Na Sisi hatukuwadhulumu
kwa kuwaharimishia hayo, lakini wamejidhulumu wenyewe kuyasabibisha hayo
kwa kupita mipaka na ushari wao, na kuacha kusimama kwenye yalio halali...
Rudi kwenye Sura
119. Kisha wanao tenda maovu kwa kupitikiwa, au kwa kuacha kuzingatia
vilivyo matokeo yatayo tokea, na baadae wakatubia, wakajitengeneza nafsi
zao na vitendo vyao, basi hakika Mola wako Mlezi, ewe Nabii, atawasamehe
hao madhambi yao. Kwani hakika Yeye Subhanahu baada ya toba hiyo ni Mwingi
wa kusamehe madhambi, na ni Mkunjufu wa rehema kwa waja wake.
Rudi kwenye Sura
120. Hakika Ibrahim, mnaye tafakhari naye nyinyi washirikina na Mayahudi,
alikuwa amekusanya kila fadhila njema, na yu mbali na upotovu wenu, ni
mt'iifu wa amri ya Mola wake Mlezi, na wala hakuwa mshirikina kama nyinyi.
Rudi kwenye Sura
121. Alikuwa mwenye kushukuru kwa neema za Mola wake Mlezi. Na kwa
haya yote ndio Mwenyezi Mungu alimteua ili abebe Ujumbe wake, na akamwezesha
kufuata Njia ya Haki Iliyo Nyooka yenye kufikilia kwenye neema ya kudumu.
Rudi kwenye Sura
122. Na tumemjaalia duniani atajike vyema, na hakika Akhera atakuwa
miongoni mwa watu wema wanao neemeshwa kwa Pepo za Allah na radhi zake.
Rudi kwenye Sura
123. Ewe Nabii! Baada ya Ibrahim kwa karne nyingi, tulikupa Wahyi
wewe, na tukakuamrisha umfuate Ibrahim katika wito wake wa kulingania Tawhid,
na fadhila njema, na kujiepusha na dini za uwongo. Kwani yeye hakuwa katika
wanao mshirikisha Mwenyezi Mungu, kama wanavyo msingizia hawa washirikina.
Rudi kwenye Sura
124. Wala sio kuitukuza siku ya Ijumaa na kuiacha Jumaamosi kama
ilivyo katika Uislamu kuwa ni kukhitalifiana na alivyo kuwa akifanya Ibrahim,
kama wanavyo dai Mayahudi. Kwani kuharimishwa kuvua (na kufanya kazi nyengine)
siku ya Jumaamosi, ndio Siku ya Sabato, kwa sababu ya kuitukuza haikuwamo
katika sharia ya Ibrahim. Hayo walilazimishwa Mayahudi tu (ambao hata hawakuwapo
zama za Ibrahim). Na juu ya hivyo hawakuitukuza, bali baadhi yao waliacha
kutukuza huko, na wakenda kinyume na amri ya Mola wao Mlezi. Basi yawaje
hata wanawatia makosani wengine kwa kutolazimishwa kutukuza jambo ambalo
wao walio lazimishwa wameliasi? Ewe Nabii! Kuwa na yakini kuwa Mola wako
Mlezi atawahukumu hao Siku ya Kiyama katika hayo mambo wanayo khitalifiana
kwayo, na atamlipa kila mmoja wao kwa vitendo vyake.
Rudi kwenye Sura
125. Ewe Nabii! Lingania, uwite watu kwenye Njia ya Haki ambayo Mola
wako Mlezi amewataka watu wako waifuate. Na katika huo Wito wako pita njia
ambayo inamnasibu kila mmoja wao. Waite wenye vyeo vya juu katika wao kwa
maneno ya hikima kwa mujibu wa akili zao. Na watu wa kawaida walio baki
kati yao walinganie kwa kuwapa mawaidha yanao waelekea, na kuwapigia mifano
ya mambo wanayo pambana nayo ya kuwapeleka kwenye Haki, na uwaongoze kwenye
njia fupi inayo wanasibu. Na jadiliana na watu wa dini zilizo tangulia
katika watu wa Biblia, yaani Mayahudi na Wakristo, kwa kutumia hoja za
kiakili, Mant'iqi, na maneno laini, na majadiliano mazuri, si maneno ya
ukali na matusi, ili uwakinaishe na uwavutie. Hii ndiyo njia ya Daa'wa
(Wito), kuwaita watu kumwendea Mwenyezi Mungu -watu wa mila zote. Basi
ifuate njia hii unapo waita, na baada ya hayo yaliyo baki mwachilie Mola
wako Mlezi, ambaye anamjua aliye zama katika upotovu kati yao na akawa
mbali na njia ya uwokovu, na nani ambaye aliye salimika, akaongoka, na
akayaamini hayo uliyo waletea.
Rudi kwenye Sura
126. Enyi Waislamu! Mkitaka kuwaadhibu wale wanao kufanyieni uadui
wakakuvamieni, basi waadhibuni kwa kadiri walivyo kutendeeni, wala msizidishe
kuliko hivyo. Na kuweni na yakini kwamba mkistahamili, msijilipizie kisasi,
itakuwa ni kheri zaidi kwenu hapa duniani na Akhera. Basi toeni adhabu
kwa ajili ya Haki, wala msiadhibu kwa ajili ya nafsi zenu.
Rudi kwenye Sura
127. Na ewe Nabii! Subiri! Kwani hivyo ndio yatakusahilikia mengi
katika mashaka ya maisha, na yataondoka matatizo yake. Wala usisikitike
kwa kuwa watu wako hawaitikii Wito wako, na hawakuamini. Wala usione dhiki
kifuani mwako kwa hila zao na vitimbi vyao vya kuukaba roho Wito wako.
Kwani vitendo vyao havitakudhuru kitu. Na wewe umekwisha tekeleza waajibu
wako, na umemcha Mola wako Mlezi.
Rudi kwenye Sura
128. Kwani hakika Mola wako Mlezi yu pamoja na wale wanao jikinga
na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kuyaepuka anayo yakataza, na wakazifanya
a'mali zao ziwe nzuri kwa sababu ya Mwenyezi Mungu kwa kukubali kumt'ii.
Yeye atawanusuru duniani, na Akhera atawalipa bora ya malipo.
Rudi kwenye Sura